January 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mashine ya CT-Scan Bugando yaharibika

Spread the love

MASHINE ya CT-Scan katika hospitali ya Rufaa Bugando (BMC) imeharibika na kusababisha wagonjwa wanaofika hospitalini hapo kukosa huduma. Anaandika Moses Mseti, Mwanza … (endelea).

Hivi karibuni Rais John Magufuli, alifanya ziara ya kushtukiza katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili na kukuta baadhi ya mashine ikiwamo ya uchunguzi wa magonjwa (MRI) zikiwa hazifanyi kazi.

Rais Magufuli katika ziara hiyo aliuagiza uongozi wa Muhimbili kuhakikisha mashine ya MRI inafanya kazi, hata hivyo baada ya siku moja ilianza kuhudumia wagonjwa kabla ya Novemba 16 kuharibika tena.

Hata hivyo katika ziara hiyo ya Rais Magufuli, Wizara ya Fedha ilitenga fedha kwa ajili ya matengenezo ya mashine zote nchini za MRI na CT-Scan ili kufanyiwa matengezo na kutoa huduma kwa wananchi.

Katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando ya Jijini Mwanza, mashine ya CT-Scan imehalibika, ambapo baadhi ya wagonjwa waliaofika hospitalini hapo wakitoka mikoa ya jirani wakikosa huduma.

Uchunguzi uliofanywa na MwanaHALISI Online, umebaini kuwa mashine ya CT-Scan katika hospitali hiyo imefanya kazi kwa miaka 15 licha ya kutakiwa kutumika miaka 10 kitendo ambacho kinadaiwa kuwa chanzo cha kuharibika kwake.

Mmoja wa wagonjwa waliofika Bugando na kukosa huduma hiyo, Chacha Mwita, huku akizungumza kwa taabu, amesema kitendo cha hospitali hiyo kukosa kifaa hicho kitasababisha wananchi wengi maisha yao kuwa hatalini.

Mwita ambaye ni mkazi wa mkoani Mara, amesema baada ya kufika bugando aliambiwa mashine hiyo imeharibika na Novemba 13 mwaka huu aliandikiwa barua akatibiwe katika hospitali nyingine za binafsi.

“Mimi nilitokea Mara, baada ya kuanguka kutoka kutoka kwenye gari, kama unavyoniona hapa, sasa kufika Bugando nikaambiwa mashine imehalibika, nilikata kurudishwa nyumbani lakini nikaandikiwa barua nikatibiwe hospitali nyingine,” amesema Mwita.

Mkurugenzi Mtendaji katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando (BMC), Kien Mteta, alipotafutwa kuzungumzia tukio hilo kupitia simu yake ya mkononi hakuipokelewa, pia alipotumiwa ujumbe wa maneno ulioeleza suala hilo haukujibiwa.

error: Content is protected !!