Saturday , 10 June 2023
Home Kitengo Michezo Mashindano Miss EAC kufanyika Tanzania
Michezo

Mashindano Miss EAC kufanyika Tanzania

Jolly Mutesi, Makamu wa Rais wa Miss East Africa 2021
Spread the love

 

MASHINDANO ya Miss East Africa 2021, yanatarajiwa kufanyika Novemba 2021 nchini Tanzania. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Nchi 16 tayari zimedhibitisha kushiriki mashindano hayo ambayo mara ya mwisho kufanyika Tanzania, ilikuwa mwaka 2012.

Taarifa kwa umma, iliyotolewa leo Jumanne, tarehe 15 Juni 2021 na Jolly Mutesi, Makamu wa Rais wa Miss East Africa 2021 imesema, hii ni fursa kwa kampuni mbalimbali zinazohitaji kutangaza biashara zao kwa ndani nan je ya mipaka ya Tanzania kupitia katika mashindano haya makubwa ya urembo.

Amezitaja nchi hizo kuwa ikiwemo Tanzania ni; Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Ethiopia, Eritrea, Djibouti, Somalia, Madagascar, Malawi, Seychelles, Sudan Kusini, Comoros, Reunion na Mauritius.

Jolly ambaye yupo Tanzania kwa ajili ya maandalizi ya mashindano hayo amesema, mashindano hayo ndiyo makubwa ya urembo kwa ukanda wa Afrika na yanatarajiwa kuangaliwa na watu wengi duniani kupitia kwenye matangazo ya moja kwa moja ya televison hivyo kutoa nafasi nzuri ya kutangaza utalii wa Tanzania pamoja na kuonyesha fursa mbalimbali za uwekezaji

Amesema, mashindano ya Miss East Africa yalibuniwa na kuanzishwa na Mtanzania, Rena Callist na kufanyika kwa mara ya kwanza mwaka 1996 kwa mafanikio makubwa, Dar es Salaam, ambapo pia yamewahi kufanyika katika nchi ya Burundi kwa udhamini wa Rais wa Burundi wa wakati huo Hayati Rais Piere Nkurunzinza

Jolly amesema, mashindano ya mwisho kufanyika ilikuwa ni mwaka 2012 ambapo yalifanyika katika ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es salaam na kuangaliwa na mamilioni ya watu Duniani kote kupitia matangazo ya moja kwa moja “Live” ambapo yalitangaza utalii wa Tanzania kwa kiasi kikubwa.

“Kuanzia sasa mashindano ya Miss East Africa yatakuwa yakifanyika kila mwaka ambapo yatasaidia sana katika kudumisha umoja wa Afrika mashariki, kukuza utalii, kutangaza fursa mbalimbali za uwekezaji hasa katika nchi inayoandaa mashindano hayo.”

“Pia kutoa elimu na kusaidia katika changamoto mbalimbali hasa zinazowakabili wanawake na watoto wa ukanda huu wa Afrika ya Mashariki.

Jolly amesema, mashindano ya Miss East Africa yanaandaliwa na kampuni ya Rena Events Limited ya Jijini Dar es salaam, Tanzania.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

MichezoTangulizi

Benki ya NBC yakabidhi kombe la ubingwa wa ligi kuu kwa Yanga

Spread the loveMDHAMINI Mkuu wa ligi ya NBC, Benki ya Taifa ya...

HabariMichezo

Benki ya NBC yazindua kombe jipya la Ligi Kuu Tanzania Bara

Spread the loveMDHAMINI Mkuu wa Ligi ya NBC , Benki ya Taifa...

MichezoTangulizi

Yanga malizeni ugomvi na Fei Toto – Rais Samia

Spread the love  RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia...

Michezo

Samia aipongeza klabu ya Yanga kwa hatua iliyofikia

Spread the love RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia...

error: Content is protected !!