SERIKALI ya Uingereza, imelegeza masharti iliyoweka kwa ajili ya kudhibiti maambukizi ya ugonjwa wa homa kali ya mapafu, inayosababishwa na Virusi vya Corona (Covid-19). Inaripoti BBC…(endelea).
Kwa sasa nchi hiyo imeondoa zuio la mikusanyiko ya watu, matukio ya kijamii, pamoja na kuruhusu sherehe za usiku. Huku uvaaji barakoa ukiwa sio lazima.
Uamuzi wa masharti hayo kulegezwa, ulitolewa jana tarehe 19 Julai 2021 na Waziri Mkuu wa Uingereza, Boris Johnson.
Waziri Mkuu huyo wa Uingereza, alisema sasa ni muda sahihi kwa Taifa hilo kurudi katika utaratibu wa maisha bila ya watu kuwekwa karantini.

Mbali ya kulegeza masharti hayo, Johnson aliwataka wananchi kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa huo.
“Lakini tunatakiwa kufanya kwa uangalifu, tunatakiwa kukumbuka kwamba virusi hivi kwa bahati mbaya viko nje, visa vinaongezeka. Tunaweza kuona maambukizi ya kirusi cha Delta yakiwa katika kiwango kikubwa,”alisema Johnson.
Waziri wa chanjo nchini humo, Nadhim Zahawi, alisema asilimia 90 ya watu wenye matatizo ya kiafya, wamepatiwa chanjo ya Covid-19.
Leave a comment