August 13, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mashahidi wawili wamtetea Kubenea

Spread the love
MASHAHIDIwawili leo wamemtetea Sead Kubenea, Mbunge wa Jimbo la Ubungo kwamba, hakutoa lugha ya matusi, anaandika Faki Sosi.
Katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam mashahidi hao wameieleza mahakama hali halisi ya tukio lililosababisha mvurugano kati ya Kubenea na Paul Makonda, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni.
Shahidi wa kwanza alikuwa Shabani Matutu, Mwandishi wa Habari kwenye Gazeti la Mtanzania chini ya Kampuni ya uchapishajia ya New Habari.
Matutu aliieleza mahakama wakati akitoa ushahidi wake kuwa, hakumsikia Kubena akitoa lugha ya matusi dhidi ya Makonda. Alisema hayo wakati akijibu maswali ya Peter Kibatala, wakili wa upande wa utetezi.
Kibatala: Siku ya 14 Desemba inahusika vipi na majukumu yako?.
Matutu: siku hiyo niliagizwa na ofisi yangu niende Mabibo kwenye Kiwanda cha TOOK ambapo kulikuwa kuna mgomo wa wafanyakazi.
Kibatala: Ni mtu au watu gani uliwaona kwenye eneo hilo?
Matutu:Nilimuona Saed Kubena, Mbunge wa Jimbo la Ubungo akifanya taratibu za kutatua mgogoro huo.
Kibatala:Unaiambia nini mahakama kuhusu uwepo wa Paul Makonda kwenye tukio hilo?
Matutu: Makonda alikuja saa 9.
Kibatala: Nini kifutaata baada kuwasili kwa Paul Makonda?
Matutu:Walewalikuwa kwenye mkutano ambao ni Saed Kubenea, uongozi wa kiwanda na viongozi wa wafanayakazi walitoka nje na baadaye wakaenda naye Makonda ndani ingawa hawakuka sana, tuliwaona wakitoka na kuelekea walipo wafanyakazi ambapo ni nje ya jengo la utwala la kiwanda hicho.
[highlight][/highlight]
Kibatala:Nini kiliendelea baada ya kwenda walipo wafanyakazi?
Matutu: Makonda alipewa kipaza sauti na kuwataka wafanyakazi saba waongee na wakaongea wafanyakazi hao, baadaye akarudishiwa kipaza sauti hicho Makonda na kusema kuwa, mkutano umeisha na yeye ndiye Rais wa Kinondoni, akizungumza yeye hatakiwi mtu mwengine kuongea.
Kibatala:Nini Kilifuatia baada ya hapo.?
Matutu:Kubenea alilamika kuwa kwanini hakupewa nafasi ya kuongea na wananchi ambao walimchagua kwa kura  zaidi ya 87 elfu na kwamba yeye sio ‘mvamizi’ kwenye mkutano huo na wala sio ‘mjinga’ kwani yupo tangu asubuhi.
Kibatala: baada Kubenea kutamka maneno hayo nini kilifuata.?
Matutu: Makonda ambaye alikuwa anaondoka alirudi na kumuliza Kubenea kwa ‘hiyo mimi mjinga’ Kubenea akijibu kuwa sijasema wewe mjinga bali nilisema mimi sio mjinga ambapo Makonda aliwaamuru askari polisi wamkamate Kubenea.
Kibatala: Ni tukio gani ambalo unalikumbaku zaidi?
Matutu:Kunyang’anywa kamera mwandishi mwezetu na kukamatwa.
Kibatala: Kwa nini unakumbuka tukio hilo.?
Matutu: Ni kwasababu mimi ni mwandishi na ipo siku nami nitakamatwa.
Kishenyi Mutalemwa, Wakili wa Serikali naye alimuuliza shahidi huyo kama ifuatavyo;-
Mutalemwa: Ulianza kazi ya uandishi lini
Matutu: Nini Miaka mitano kwenye uandishi wa habari.
Mutalemwa: Ulisema kuwa wewe unakumbuka tukio la kunyang’anywa kamera kwa mwandishi mwenzako, je unamkumbuka alikuwa nani.?
Matutu: Simkumbuki.
Mutalemwa: Ulisesema kuwa hakusikia matusi ni sahihi.
Matutu: Ni sahihi.
Katika upande wa mshitakiwa kulikuwa kuna shahidi mwengine alijitambulisha kama Josephat Isango ambaye pia ni Mwandishi wa Habari. Mahojiano yake na wakili  kwenye mahakama hiyo yalikuwa  kamaifuatavyo.
Kibatala: Wewe ni mwandishi wa gazeti gani
Isango:MwanaHALALISI.
Kibatala: Ulikuwa wapi siku ya 14 Desemba 2015?
Isango: Mapema asubuhi nilikuwa ofisini lakini baadaye nikaarifiwa na mhariri niende eneo la Mabibo ambapo kulikuwa kuna mgomo wa wafanyakazi.
Isango alieleza mahakama kuwa, alikuwa katikati ya Kubenea na Makonda, baada Kubenea kumwambia kuwa yeye sio kibaka na wala sio mjinga Makonda alirudi kwa kasi na  kueleza kuwa, alimsukuma yeye na kumwambia Kubenea imanaana mimi ni mjinga?
Amesema, Kubenea alijibu kuwa mimi nimesema kuwa mimi sio mjinga na sijasema wewe mjinga.
Isango aliendelea kuileza mahakama kuwa, Makonda alimuru askari polisi wamkamate Kubenea ambapo maagizo hayo alipewa afande Denis.
Afande Denisi aliiagiza polisi wengine wamkamate Kubenea kwani yeye alikuwa anashughilika na Mwandishi wa Star TV aliyekuwa na kamera ambayo alimnyang’anya. Hata hivyo alisema hakusikia Kubenea akimtolea lugha ya matusi.
Kishenyi Mutalemwa,Wakili wa Serikali alipewa nafasi ya kumuhoji Isango.
Mutalemwa: Kubenea ni mwandishi pia ni Mkurugenzi wa MwanaHALISI.
Isaingo: Ndio.
Mutalemwa:Uliieza mahakama kuwa wewe unafanaya kazi chini ya mhariri, je unaweza kumuandika vibaya mkurugenzi wako?.
Isango: Mkuregenzi tunaweza kuripoti akifariki au akifanya jambo baya kwani ni kanuni za uandishi na kwamba, nisipomuandika mimi waandishi wengine watamuandika.
Mutalemwa: Je, mpiga picha wa Star TV aliondoka na nani?
Isango: Naithibitishia mahakama kuwa aliondoka na Denis.
Mutalemwa: Je ulifuatilia tukio la kunyang’anywa kamera kwa mwandishi mwenzenu.?
Isango: Ndio nilifutilia mpaka kituoni ambapo afande Denis alikata kutoa kamera.
Ushahidi wa kesi hiyo umeshasikilizwa pande zote mbili na kwamba, Thomas Simba, Hakimu Mkazi Kisutu amewataka makili wa pande zote mbili kupeleka hoja kwa njia ya maandishi tarehe 18 Machi na baadaye itapangiwa siku ya maamuzi ya kesi hiyo.
error: Content is protected !!