September 25, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Mashabiki Yanga njia Panda kushuhudia mchezo Ligi ya Mabingwa.

Spread the love

IKIWA zimebakiwa siku tano kuelekea mchezo wa hatua ya awali wa Ligi ya Mabingwa Afrika, kati ya Yanga dhidi ya Rivers United, hatma ya mashabiki kuingia katika mchezo huo bado haijafahamika kutokana na wenyeji kutopewa taarifa mpaka sasa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Barani Afrika (CAF). Anaripoti Kelvin Mwaipungu …(endelea)

Mchezo huo utapigwa jumapili hii ya Septemba 12, majira ya saa 11 jioni, kwenye dimba la Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.

Akizungumza moja ya kituo cha Radio leo Asubuhi, Afisa Habari na mawasiliano wa klabu ya Yanga, Hassan Bumbuli amesema kuwa mpaka sasa hawajapokea taarifa yoyote ya kuruhusiwa kuingiza mashabiki kwenye mchezo na kama wataipata muda wowote watawatangazia mashabiki zao.

“Kuhusu mashabiki mpaka sasa hatujapata taarifa yoyote kutoka Caf, kama wataruhusiwa au kuzuiliwa, kama tuliruhusiwa na kwa idadi gani basi tutawaambia, na kama hatujaruhusiwa tutaomba watuunge mkono huko huko walipo.” Alisema Bumbuli

Yanga inarejea tena kwenye michuano ya kimataifa mara baada ya kukaa nje kwa msimu mmoja, mara baada ya mara ya mwisho kutolewa na Zesco United ya nchini Zambia kwenye michuano ya kombe la Shirikisho Barani Afrika kwenye msimu wa 2021.

Hassan Bumbuli, Afisa Habari wa klabu ya Yanga

Aidha katika hatua nyingine Afisa Habari huyo alikana taarifa zinazoendelea kwenye mitandao ya kijamii ya kwamba wapinzani wao Rivers United tayari wameshaingia nchini kwa jili ya mchezo huo.

“Taarifa hizo sio za kweli wapinzani wetu Rivers United kwa mawasilano tuliofanya nao, wanatarajia kuingia nchini siku ya Alhamic Usiku au Ijumaa Asubuhi kwa ajili ya mchezo huo” alisistiza Afisa Habari huyo

Yanga imepata tiketi ya kushiriki michuano hiyo, mara baada ya Tanzania kupata nafasi ya ushiriki wa timu nne, kwenye michuano ya kimataifa mwaka huu, huku timu mbili za zikishiriki michuano ya Shirikisho na mbili michuano ya klabu bingwa.

Mara baada ya mchezo wa Septemba 12, 2021jijini Dar es Salaam, mchezo wa marudiano utapigwa Septemba 19, nchini Nigeria.

error: Content is protected !!