February 27, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Mashabiki wavamia nyumba ya mchezaji Zambia

Timu ya Taifa ya Zambia

Spread the love

POLISI nchini Zambia wamewakamata mashabiki watano kwa madai ya kuvamia nyumba ya mwanasoka wa timu ya taifa ya kandanda, Alex N’gonga.

Mashabiki hao walishikwa na hasira kuwa Ng’onga alikosa nafasi wazi za kufunga wakati wa mechi muhimu ya kufuzu kwa kombe la dunia ambapo Nigeria iliishinda Zambia bao 1-0

Mashabiki walitoa hasira zao kwa kuvamia nyumba yake iliyo mji wa Kitwe ambao waliitupia mawe na kwa mujibu wa kamishina wa polisi, Charity Katanga.

“Tumekamata watu watano kwa makosa ya kuharibu mali na sasa wanazuiliwa na polisi.”

Kushindwa kwa Zambia kuliipokonya fursa ya kufuzu kwa kombe la dunia nchini Urusi ambapo Nigeria walifuzu.

error: Content is protected !!