January 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Masele ajitosa kumrithi Ndugai

Spread the love

 

ALIYEWAHI kuwa Mbunge wa Shinyanga Mjini (CCM), Stephen Masele amechukua fomu za kuwania Uspika wa Bunge la Tanzania. Anaripoti Mwandishi Wetu..(endelea).

Masele aliyewahi kuwa Makamu wa Rais wa Kwanza wa Bunge la Afrika (PAP), amechukua fomu hiyo leo Jumatatu, Ofisi za CCM Lumumba jijini Dar es Salaam.

Ni baada ya CCM kutangaza mchakato huo wa uchukuaji na urejeshaji fomu kuanzia leo hadi 15 Januari 2022 ili kujaza nafasi iliyoachwa wazi na Job Ndugai ambaye alitangaza kujizulu 6 Januari 2022.

Masele amewahi kuwa Naibu Waziri wa Nishati na Madini katika utawala wa awamu ya nne wa Jakaya Kikwete.

Fomu hizo zinatolewa ofisi za Lumumba, Dar es Salaam, Makao Makuu CCM Dodoma pamoja na Kisiwandui visiwani Zanzibar.

error: Content is protected !!