September 29, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Masauni: Magereza kuchangia uchumi wa kati

Spread the love

SERIKALI imesema, italitumia Jeshi la Magereza nchini katika kutekeleza azma yake ya kuingia katika  uchumi wa kati ambao utachangiwa na uanzishwaji wa viwanda kwa kuendeleza miradi mbalimbali ambayo imeanzishwa na jeshi hilo, anaandika Dany Tibason.

Kauli hiyo imetolewa leo na Hamad Masauni, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi wakati alipotembelea mradi wa uzalishaji wa madini ya ujenzi katika Gereza la Msalato, Dodoma.

Amesema kuwa, miradi mingi ambayo inaendeshwa na jeshi hilo nchini kama serikali itasaidia katika kuiwezesha, italisadia taifa katika kupiga hatua na kuingia katika uchumi wa viwanda.

“Kwa mradi kama huu tulio ukuta hapa wa kuzalisha madini ya ujenzi tukiwekeza fedha tutaweza kuongeza pato la serikali kutoka na mahitaji yaliyopo kwajili ya ujenzi wa makazi na miundombinu mbalimbali,” amesema Masauni.

Amesema kuwa, umefika wakati wa jeshi hilo kujitegemea lenyewe kwa kutumia miradi mbalimbali inayotekelezwa na jeshi hilo sambamba na kuinua uchumi wa taifa.

“Ni wakati sasa wa kuacha kufanya kazi kwenye maandishi umefika sasa wakati wa utekelezaji wa miradi mbalimbali ambayo imepangwa kwenye maandishi na kuanza kuitekeleza kwa uharisia, na sasa inaanza kuonekana utekelezaji huo kupitia Jeshi la Magereza la Msalato,” amesema.

Amesema katika mradi huo wa mawe Msalato serikali inatakiwa kuwekeza kiasi cha Sh. 2.8 bilioni ambazo zitatumika kununua vifaa mbalimbali vya uchakataji wa kokoto na kila mwaka mradi huo utakuwa na uwezo wa kuingiza faida ya Sh. 6.8 bilioni  faida.

“Kama serikali itakubali kutupatia kiasi hicho cha fedha basi tutaweza kuingiza faida ya Sh. bilioni sita kwa mwaka wa kwa na na baada ya mika kumi itakuwa faida ni mara mbili,” amesema Masauni.

Masauni ameongeza kuwa, pamoja na mradi huo kuwekewa msisitizo katika kuuboresha pia watahakikisha wanaendeleza miradai mingine kama ile ya uzalishaji wa viatu.

“Hata ukiangalia majeshi yetu karibu yote yanaangiza viatu kutoka nje jambo hili ni aibu sana hivyo basi serikali ya awamu ya tano itahakikisha inaiendeleza miradi hii yote ambayo ipo chini ya jeshi la magereza nchini,” amesema.

Kwa upande wake mrakibu msaidizi wa magereza (ASP) Patrick Nasola, amesema kuwa mradi huo wa kuzalisha madini ya ujenzi unauwezo wa kuzalisha tani 20 kwa siku za kokoto.

“Kama tutapata pesa za kurekebisha mashine yetu ya kuzalisha kokoto ambayo imeharibika kwa sasa na tulikuwa tunatarajia kuanza kuwauzia watu wanao jenga uwanja wa ndege”amesema Nasola.

error: Content is protected !!