October 3, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Masauni awanyoshea kidole kampuni za Ulinzi

Spread the love

SERIKALI imesema kuwa inazo taarifa kuwa yapo baadhi ya makampuni binafsi ya ulinzi ambayo yanajihusisha na vitendo vya uhalifu nchini. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Pamoja na baadhi ya walinzi wa kampuni za ulinzi binafsi kujihusisha na mambo ya uhalifu bia serikali imeeleza kuwa wapo baadhi ya walinzi wa kampuni hizo kukodisha siraha kwa ajili ya kufanyia uhalifu.

Kauli hiyo ilitolewa jana na Naibu Waziri wa Manbo ya Ndani ya Nchi,Hamad Masaun katika ufunguzi wa mkutano mkuu wa Chama cha Sekta ya Ulinzi Tanzania (TSIA) uliofanyika Jijini Dodoma.

Katika ufunguzi wa Mkutano huo Masaun alisema kuwa serikali inazo taarifa za baadhi ya walinzi wa Kampuni mbalimbali za ulinzi kuhusika na matukio ya uhalifu hapa nchini na baadhi ya walinzi wamekuwa wakidiriki kuwahazima silaha wahalifu kwenda kufanyia uhalifu.

Kutokana na hali hiyo Masauni alisema jambo hilo halikubaliki na kutoa agizo kwa kampuni zenye walinzi wa aina hiyo kuhakikisha vitendo hivyo vinakoma mara moja.

Hata hivyo Masaun alibainisha kuwa Makampuni mengi ya ulinzi binafsi hayajali masilahi ya watumishi wao jambo ambalo linasababisha walinzi kukata tama na kujikuta wanarubuniwa na watu wenye nia ovu hususani majambazi.

“Katika kuboresha huduma ya ulinzi jambo la kwanza ni kuangalia maslahi ya watumishi wenu, bila kuwa na maslahi mazuri wafanyakazi hukata tama na hivyo kuwa rahisi kwao kurubuniwa na kujiingiza katika vitendo vya uhalifu.

“Aidha wanaweza kutumika katika kudhoofisha kampuni kwa kufanya uzembe wa makusudi na kusababisha wizi na hasara katika Kampuni, tunazo taarifa ya baadhi ya walinzi wa Kampuni mbalimbali za ulinzi kuhusika na matukio ya ualifu hapa nchini.

“Pia baadhi ya walinzi wamediriki kuwaazima silaha wahalifu kwenda kufanyia uhalifu,jambo hili halikubaliki ,na ninaagiza kampuni zenye walinzi wa aina hii kuhakikisha vitendo hivyo vinakoma mara moja,” alisema Masaun.

Katika hatua nyingine aliwataka wamiliki wa Makampuni ya ulinzi kuhakikisha wanakuwa makini na matumizi ya siraha, utunzaji wa silaha mahali panapofaa na kueleza kuwa kama kutakuwepo na uzembe kunawezekana kukawa chanzo cha silaha kuingia mikononi mwa watu wasio kuwa waaminifuhasa majambazi na kuogeza tatizo la uhalifu.

Masauni akizungumzia utendaji unaofuata sheria na haki za binadamu, alisema kwamba katika kupambana na uhalifu ni lazima zifuatwe sheria na haki za binadamu.

“Katika kupambana na uhalifu naomba tuzingatie sheria za haki za binadamu, kuna mazoea ya watu kujichukulia sheria mikononi kwa kuwaadhibu watuhumiwa wanapokamatwa kwa kisingizio cha hasira kali, vitendo hivi vinakinzana na dhana nzima ya utawala wa sheria,” alieleza Masauni.

error: Content is protected !!