Monday , 30 January 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Marufuku wanaosimamia biashara kuwa vyanzo vya mapato
Habari za Siasa

Marufuku wanaosimamia biashara kuwa vyanzo vya mapato

Rais Samia Suluhu Hassan
Spread the love

MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan amezitaka taasisi za umma zenye jukumu la kudhibiti na kusimamia biashara na mazingira, kutokuwa vyanzo vya mapato. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Mama Samia ametoa wito huo tarehe 7 Juni 2019 katika mkutano wa Rais John Magufuli na wafanyabiashara nchini , uliofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.

Mama Samia ameeleza kuwa, taasisi nyingi zimekuwa zikilalamikiwa kwamba zimeacha kutekeleza majukumu yao ya udhibiti na kuwa chanzo cha mapato.

Ameitaka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuishughulikia changamoto hiyo,ili taasisi husika zitekeleze majukumu yake kwa mujibu wa sheria.

“Taasisi za udhibiti zile zilizo lalamikiwa hapa, mwansheria uangalie, tatizo ni kwamba taasisi hizo zimekuwa vyanzo vya mapato, zimeacha kufanya kazi zao za udhibiti na kuwa chanzo cha mapato, ” amesema Mama Samia na kuongeza.

“Sheria zinaagiza kufanya udhibiti na kutoa faini kwa watakao kiuka sheria. Walioundwa kufanya udhibiti wafanye udhibiti, walioundwa kutoa huduma na kutoza tozo wafanye kazi yao.”

Huku akiitaja Wakala wa Udhibiti na Usimamizi wa Mazingira Tanzania (NEMC), Mama Samia amesema ofisi yake imeanza kuwachukulia hatua baadhi ya watumishi wa wakala huo, ambao wanakiuka sheria.

Mama Samia amesema ofisi yake imeunda kamati ya kufuatilia utendaji wa NEMC, na kwamba hadi sasa kuna vigogo watano wa wakala hao wamefikishwa katika Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kwa makosa mbalimbali ikiwemo kuchukua kodi kinyume na sheria.

“Tumeanza kuibadilisha NEMC, tuliunda kamati ya kuingalia, kuna watu si chini ya nne au watano wako chini ya TAKUKURU, kwa sasa hivi NEMC itakua inabadilika,” amesema Mama Samia.

Aidha, Mama Samia amewataka wafanyabiashara kueleza changamoto zao ili serikali izitatue.

“Ninyi ndio tegemeo letu, kuna matatizo au changamoto ni vizuri kuzielezea ili zifanyiwe kazi,” amesema Mama Samia.

Pia, Mama Samia amewataka wafanyabiashara waliohudhuria mkutano huo kufikisha mapendekezo yao kwa Rais Magufuli ili yafanyiwe kazi.

“Rais ulipendekeza wakae kesho waje na maazimio yaliyoazimiwa kwenye mkutano huu, ningeshauri mkae kwa kanda na kutoa mapendekezo yenu itakuwa rahisi kwa kuyachambua na kuyatekeleza,” amesema Mama Samia.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chongolo asikitishwa na mradi wa Mil 900 kutoanza kutoa manufaa

Spread the loveKATIBU mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa Daniel Chongolo...

Habari za Siasa

NCCR-mageuzi yawaangukia Polisi kupotea kwa kada wake

Spread the loveJESHI la Polisi nchini limeombwa kufanya uchunguzi wa kina utakaosaidia...

Habari za Siasa

Uamuzi kesi ya kupinga Bodi ya Wadhamini NCCR-Mageuzi kutolewa Februari 6

Spread the love  MAHAKAMA Kuu, Masjala Kuu ya Dar es Salaam, imepanga...

Habari za SiasaTangulizi

Lissu:Suluhu ya ugumu wa maisha ni Katiba Mpya

Spread the love  MAKAMU mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo-Chadema Bara,...

error: Content is protected !!