Friday , 29 September 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Mahakama wang’oa Wakurugenzi H’shauri, Manispaa kusimamia Uchaguzi
Habari za SiasaTangulizi

Mahakama wang’oa Wakurugenzi H’shauri, Manispaa kusimamia Uchaguzi

Spread the love

MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam imebatilisha kifungu cha sheria cha 7(3), kinayowaruhusu Wakurugenzi wa Manispaa na Halmashauri kuwa wasimamizi wa Uchaguzi nchini. Anaripoti Faki Sosi … (endelea).

Leo tarehe 10 Mei, 2019, uamuzi huo umetolewa na Jaji Utuganile Ngwala katika kesi namba 8 ya mwaka 2018, iliyofunguliwa na Bob Chacha Wangwe, Mwanachama wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

Katika maamuzi hayo, Jaji Ngwala pia ametengua kifungu cha 7 (1) kinachoruhusu mtu yeyote kuwa msimamizi wa uchaguzi.

Jaji Ngwala akisoma uamuzi huo, amesema kuwa sheria hizo ni batili na kinyume cha katiba ya nchi.

Amesema kwa mujibu wa ushahidi uliowasilishwa kwenye mahakama hiyo na muombaji kuwa wasimamizi wa chaguzi ni wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), ambao wanamaslahi kwenye chaguzi hizo.

Muombaji (Bob) amewakilishwa na Wakili Fatma Karume, kwenye kesi hiyo ambaye ametoa ushahidi wa majina 74 ya wasimamizi wa uchaguzi ambao ni wanachama wa (CCM).

Jaji Ngwala amesema kuwa sheria hizo hazijaelekeza utaratibu wowote wa kuhakiki kuwa wasimimizi hawana maslahi binafsi na uchaguzi.

Amesema ya kuwa  sheria hii ya Tume ya Uchaguzi imekataza mtu yoyote ambaye mwanachama wa chama chochote haruhusiwi kuwa msimamizi wa Uchaguzi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kapinga: Usambazaji umeme vijijini mwisho Desemba 2023

Spread the love  NAIBU Waziri wa Nishati, Judith Kapinga, amesema ifikapo mwezi...

Habari za Siasa

Mgongano wa kimasilahi wamhamisha Chande TTCL

Spread the love  ALIYEKUWA Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO),...

Habari za SiasaTangulizi

Mgawo wa umeme: Rais Samia ampa miezi sita bosi mpya TANESCO

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amempa miezi sita Mkurugenzi...

Habari za Siasa

Rais Samia avunja bodi ya REA

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amemteua Balozi Jacob Kingu, kuwa...

error: Content is protected !!