March 2, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Marufuku mkandarasi aliyeboronga kuhamia mkoa mwingine

Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Prof. Makame Mbarawa (kushoto) akiwa na Naibu wake, Januari Makamba

Spread the love

WAZIRI wa Maji na Umwagiliaji, Profesa Makame Mbarawa amepiga marufu wakandarasi wanaoharibu miradi, kuhamishiwa maeneo mengine. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Prof. Mbarawa ametoa agizo hilo leo tarehe 7 Novemba 2018 wakati akizungumza na wasimamizi wa mamlaka za maji nchini.

“Kitendo cha Mkandarasi kuharibu miradi ya kazi mkoa mmoja na akahamishiwa mkoa mwingine naomba kuanzia sasa iwe mwisho. Hatuwezi kuendelea kuwapa kazi watu ambao wameshatuharibia kazi,” amesema Prof. Mbarawa.

Katika hatua nyingine, Prof. Mbarawa amesema kuanzia sasa watendaji wa sekta ya maji watakuwa wanapimwa utendaji wao katika kutatua shida ya maji kwa wananchi wa maeneo yao, na kwamba mtendaji atakayeshindwa kufikia malengo hayo atakuwa ana hatarisha nafasi yake

error: Content is protected !!