Friday , 1 March 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Marekani yataka Qatar ilegezewe kamba
Kimataifa

Marekani yataka Qatar ilegezewe kamba

Spread the love

WAZIRI wa mashauri ya nchi za kigeni wa Marekani, Rex Tillerson anasema kuwa nchi za Ghuba ni lazima zilegeze hatua yao dhidi ya Qatar ambayo inalaumiwa na majirani zake kwa kuunga mkono Ugaidi, anaandika Hamisi Mguta.

Saudi Arabia, Muungano wa nchi za kiarabu, Misri na Bahrain walikata uhusiano wa usafiri na wa kidiplomasia na Qatar siku ya Jumatatu.

Tillerson anasema kuwa hatua hiyo inasabisha kuwepo madhara ya kibinadamu.

Licha ya kumsifu Emir wa Qatar kwa kupuuza uungwaji mkono makundi ya kigaidi, Bwana Tillerson anasema mengi yanahitaji kufanywa.

Naye Rais Trump ameishutumu Qatar kwa kufadhili ugaidi na kuitaka ikome

Awali Rais Trump alikuwa ameandika kwenye mtandao wa Twitter akiunga mkono hatua ya kuitenga Qatar, na hata kudai kuwa alishiriki katika uamuzi uliochukuliwa na Saudi Arabia pamoja na nchi zingine.

Ndege za Qatar zilipigwa marufuku ya kutumia anga za baadhi ya majirani zake.

Hatua hiyo ya ghafla ilichukuliwa baada ya msukosuko ambao umedumu miaka kadha kati ya Qatar na majirani zake wa Ghuba.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Kimataifa

Wanajeshi Ukraine waishiwa risasi, 31,000 wauawa

Spread the loveRais wa Ukraine, Volodymyr Zelenskyy amesema zaidi ya wanajeshi 31,000...

Kimataifa

Waziri mkuu Palestina ajiuzulu

Spread the loveWaziri Mkuu wa Palestina, Mohammed Shtayyeh ametangaza kujiuzulu pamoja na...

Kimataifa

Rais mstaafu ahukumiwa miaka 4 jela

Spread the loveMahakama ya mjini Tunis imemhukumu rais wa zamani wa Tunisia,...

Kimataifa

Malawi yaondoa vikwazo vya viza kwa nchi 79 ikiwamo TZ

Spread the loveWaziri wa usalama wa ndani nchini Malawi, Ken Zikhałe ametangaza...

error: Content is protected !!