Saturday , 20 April 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Marekani yapata Spika baada ya kura kurudiwa mara 15 kwa siku 4
Kimataifa

Marekani yapata Spika baada ya kura kurudiwa mara 15 kwa siku 4

Kevin McCarthy
Spread the love

 

KEVIN McCarthy amechaguliwa kuwa Spika wa Baraza la Wawakilishi la Marekani huku kukiwa na majibizano makali ambayo karibu yashuhudiwe wawakilishi wa chama chake cha Republican washikane mashati. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa … (endelea).

McCarthy hatimaye ameshinda nafasi hiyo baada ya duru 15 za upigaji kura, licha ya chama chake kuwa na kura nyingi katika bunge.

Ushindi wake umekuja baada ya kampeni kali ya shinikizo iliyofanywa na kushuhudiwa mubashara huku mmmoja wa waasi wa chama Matt Gaetz aliyekuwa hamuungi mkono mwanasiasa huyo alihimizwa kumpigia kura McCarthy. Congressman wa Florida alikuwa miongoni mwa watu sita ambao walijiuzulu Ijumaa.

Hapo awali, huku kukiwa na majibizano makali, Gaetz alikuwa karibu apigwe na Mwakilishi Mike Rogers – mfuasi wa McCarthy. Mbunge huyo wa Alabama alilazimika kuzuiwa na wenzake alipokuwa akimfokea na kumnyooshea kidole Bw Gaetz.

Nchini Marekani Spika wa bunge hilo huweka ajenda za Bunge na husimamia shughuli za kutunga sheria. Nafasi hiyo ni ya pili kwa ukubwa nchini Marekani kama ilivyo kwa makamu wa rais baada ya Rais wa Marekani.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

Kimataifa

Majaji kuamua hatima ya Zuma leo

Spread the loveMajaji nchini Afrika Kusini leo Jumanne wataamua ikiwa rais wa...

Habari za SiasaKimataifa

Spika Afrika Kusini ajiuzulu kwa tuhuma za rushwa

Spread the loveSpika wa Bunge la Afrika Kusini, Nosiviwe Mapisa-Nqakula ametangaza kujiuzulu...

Habari MchanganyikoKimataifa

Tetemeko la ardhi laua 7, lajeruhi 800 Taiwan

Spread the loveWatu wapatao saba wamefariki dunia na wengine zaidi ya 800...

error: Content is protected !!