UBALOZI wa Marekani nchini Tanzania umesema, Makamu wa kwanza wa Rais Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad (77), alikuwa kiongozi anayeweka mbele watu badala ya madaraka. Anaripoti Matrida Peter…(endelea)
Marekani, umemzungumzia mwanasiasa huyo mkongwe, aliyefariki dunia leo Jumatano tarehe 17 Februari 2021, Hospitali ya Taifa Muhimbili, jijini Dar es Salaam, alipokuwa amelazwa kwa matibabu.
Katika kuraza za kijamii za facebook na Twitter za ubalozi huo, umeweka picha ya Balozi wa Marekani nchini Tanzania, Dk. Donald Wright na Maalim Seif, waliyoipiga hivi karibuni.
Picha hiyo, imeambatana na maneno ya Balozi Wright akisema “ninaungana na Watanzania wote – hususan Wazanzibari – kuomboleza msiba mkubwa wa kuondokewa Maalim Seif.”
“Katika maisha yake akiwa mwanasiasa kwa zaidi ya miaka 40, Maalim Seif amekuwa kielelezo cha kiongozi mtumishi anayewaweka watu mbele kabla ya madaraka. Hatutaweza kuziba pengo lake, lakini tunaweza na ni lazima tuuenzi mchango wake adhimu,” ameandika Balozi Wright
Leave a comment