Saturday , 22 June 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Marekani yampa heshima mpya Mohammed Ali
Kimataifa

Marekani yampa heshima mpya Mohammed Ali

Spread the love

UWANJA wa Ndege wa Kimataifa wa Louisville uliopo Kentucky, Marekani sasa utabadilishwa jina na kuwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mohammed Ali. Vinaripoti vyombo vya kimataifa … (endelea).

“Tuna furaha kubwa kuueleza umma kuwa, uwanja wetu wa Ndege wa Louisville sasa utabadilishwa jina na kuwa Louisville Muhammad Ali,” taarifa hiyo imesambazwa kwenye kurasa za kijamii za mamlaka ya uwanja huo na kuripotiwa na vyombo mbalimbali vya habari vya kimataifa.

“Kuendelea kuhuisha kazi na mchango wa Muhammed Ali kama mtu muhimu na aliyezaliwa na kukulia katika mji huu ni jambo kubwa la kujivunia na lenye mapenzi makubwa kwetu,” imeeleza taarifa hiyo.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa, kufanya hivyo ni kuuelezea ulimwengu kuwa Louisville inajuvunia kuwa na mtu kama Mohammed Ali na inatambua mchango wake.

“Hii sio heshima ya mji wetu pekee tumeendeleza heshima hii kwa kubadilisha jina la uwanja wetu,” amesema Mwenyekiti wa Uwanja huo Jim Welch kwenye taarifa yake.

Mohammed Ali alizaliwa kwenye mji huo (Louisville) kukulia na kufanya shughuli zake zote za michezo na hata kufikia ndgazi ya juu kama mwanamasumbwi bora wa Dunia.

Meya wa mji huo Greg Fischer amesema, mchango wa Ali unaonekana wazi kwenye michezo na sehemu zingine ndani na nje ya mji aliokulia.

“Huyu ni mtu maarufu, amefanya mengi katika jamii yetu na yanayopaswa kuigwa. Si katika michezo peke yake hata katika mambo ya kijamii na kusababisha mabilioni ya watu kumjua na kutaka kumuiga,” amesema Meya Fischer.

Mohammed Ali alizaliwa mwaka 1964 na kupewa jina la Cassius Marcellus Clay Jr, alifariki dunia akiwa na umri wa miaka 74, baada ya kubadili dini na kuwa Muislam alijiita Mohammed.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoKimataifa

Mwanajeshi amuua mchungaji baada ya kumfuma na mkewe kitandani kwake

Spread the loveHali ya simanzi imetanda katika kijiji kimoja huko Kapsabet kaunti...

Habari za SiasaKimataifa

Mmoja afariki, 30 wajeruhiwa maandamano Kenya

Spread the loveMtu mmoja ameripotiwa kuuawa na wengine zaidi ya 30 kujeruhiwa...

Habari za SiasaKimataifaTangulizi

Ramaphosa achaguliwa tena kuwa rais Afrika Kusini

Spread the loveRais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa amechaguliwa na wabunge wa...

Habari za SiasaKimataifaTangulizi

DA, ANC waridhia kuunda serikali ya mseto Afrika Kusini

Spread the loveChama tawala nchini Afrika Kusini cha African National Congress, ANC,...

error: Content is protected !!