August 18, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Marekani yakoleza vita umiliki wa silaha

Spread the love

BUNGE la Wawakilishi nchini Marekani limeafiki kupigwa marufuku kwa Wamarekani wenye matatizo ya akili kumiliki silaha ikiwa ni jitahada za kukabiliana na uhalifu wa kutumia silaha nchini Marekani, anaandika Wolfram Mwalongo.

Utawala wa Rais Mstaafu Obama ulidhamiria kukomesha umiliki holela wa silaha nchini Marekani, hata hivyo baadhi ya Wabunge kutoka Bunge la Congress walikosoa vikali sheria hiyo kwa kile walichodai sheria hiyo ilitungwa kwaajili ya Wamrekani wote pasipo kuangalia tofauti zao. 

Bob Goodlatte, mwenyekiti wa kamati ya haki amekuwa akikosoa sheria hiyo kwa madai kwamba ni ya kibaguzi kwani hakuna ushahidi wowote unaothibitisha watu wa aina hiyo ndio wanaofanya mashambulizi ya silaha katika taifa hilo.

Itakumbukwa kuwa Donald Trump Rais aliye madarakani kwa sasa, wakati wa kampeni alisema wazi kwamba haoni tatizo la wamrekani kumiliki silaha kwani mashambulizi yanatekelezwa na magaidi. Hata hivyo Bunge la nchi hiyo limeamua tofauti na mtazamo wake.

error: Content is protected !!