September 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Marekani yajitosa ujenzi bandari ya Bagamoyo

Spread the love

SERIKALI ya Marekani imeahidi kutoa ushauri wa kitaalamu kuhusu ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo, kama Tanzania itakubali kupokea msaada huo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Taarifa hiyo imetolewa leo Alhamisi, tarehe 12 Mei 2022, jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais-Ikulu, Zuhura Yunus, akielezea mafanikio ya ziara ya kikazo iliyofanywa na Rais Samia Suluhu Hassan, nchini Marekani, Aprili mwaka huu.

“Kwa upande wa ujenzi wa Bagamoyo, Serikali ya Marekani wao wamesema iko tayari kutoa utaalamu wa ushauri kuhusu ujenzi huo wa Bandari ya Bagamoyo endapo Seriklai ya Tanzania itahitaji,” amesema Zuhura.

Katika nyingine, Zuhura amesema, Marekani imeridhishwa na hali ya kisiasa iliyopo nchini, na kwamba imeahidi kuendelea kushirikiana na Tanzania katika masuala hayo.

“Nchi ya Marekani wameridhishwa na hali ya kisiasa inavyoendelea nchini, hivyo wanaona ni muhimu kuendelea kushirikiana na Tanzania kwenye mambo hayo,” amesema Zuhura.

Ujenzi wa bandari hiyo ulizinduliwa 2015 na Serikali ya Awamu ya Nne, chini ya Rais Jakaya Kikwete, lakini Juni 2019, Serikali ya Awamu ya Tano, chini ya Rais Hayati John Magufuli, ulisitisha utekelzaji wa mradi huo uliokuwa chini ya mradi wa ukanda maalumu wa kiuchumi wa Bagamoyo.

Mradi huo ulikuwa ukifadhiliwa na Serikali ya China, ulisitishwa na Rais Magufuli kwa maelezo kwamba mkataba wake ulikuwa wa hovyo.

Hata hivyo, Serikali ya Awamu ya Sita, chini ya Rais Samia Suluhu Hassan, umefufua majadiliano kuhusu ujenzi wa mradi huo na wawekezaji.

error: Content is protected !!