Saturday , 2 December 2023
Home Kitengo Habari Kimataifa Marekani yaikomalia Afghanistan, yasitisha misaada
Kimataifa

Marekani yaikomalia Afghanistan, yasitisha misaada

Donald Trump
Spread the love

MISAADA  ya kiusalama kwa Pakistan yenye thamani ya takriban dola milioni 900 itasitishwa hadi pale Pakistan itakapochukua hatua madhubuti ya kupambana na kundi la wanamgambo wa Afghanistan la Taliban na la Haqqani.

Hatua hiyo ilitangazwa na Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani huku ikisema Rais Donald Trump amekerwa na  Pakistan kushindwa kuchukua hatua za kutosha dhidi ya makundi hayo mawili ambayo yamekuwa yakiitumia nchi hiyo kama sehemu ya kujificha na kufanya mashambulizi katika nchi jirani ya Afghanistan.

Ufadhili huo utakaositishwa utaathiri ununuzi wa vifaa vya kijeshi, mafunzo, huduma nyingine za kijeshi na mpango wa kupambana na ugaidi.

Akiwahutubia wanahabari, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje wa Marekani,  Heather Nauert amesema hatua hiyo ya kusitisha ufadhili, haitaathiri misaada inayotolewa kwa raia wala ile ya kusaidiai uchumi wa Pakistan.

Nauert amesema fedha hizo huenda zikaidhinishwa kutolewa iwapo Pakistan itachukua hatua zinazostahili kukabiliana na makundi ya kigaidi.

Bunge la Marekani limefahamishwa kuhusu uamuzi huo wa kustishia misaada kwa Pakistan.

Pakistan kwa muda mrefu imekanusha shutuma kuwa imeshindwa kupambanana na makundi ya wanamgambo yanayopambana dhidii ya majeshi ya Afghanistan na ya kigeni kutokea upande wa pili wa mpaka.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Kimataifa

Israel yarejesha mashambulizi Gaza ikilaumu Hamas kukiuka makubaliano

Spread the loveJESHI la Israel, limerejesha mashambulizi katika ukanda wa Gaza, baada...

Kimataifa

Papa Francis kumfukuza Kardinali anayepinga mageuzi Kanisa Katoliki

Spread the loveKIONGOZI wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Francis, anadaiwa kupanga kumfumkuza...

Kimataifa

Mateka wa Israel, Gaza kuanza kuachiwa leo

Spread the loveMakubaliano ya kusitisha mapigano kati ya Israel na vikosi vya...

Kimataifa

Israel, Hamas kusitisha mapigano kwa muda

Spread the loveNCHI ya Israel, pamoja na kikundi cha wanamgambo wa kiislamu,...

error: Content is protected !!