Thursday , 25 April 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Marekani yaghairi kuichapa Iran, kuiwekea vikwazo kiuchumi
Kimataifa

Marekani yaghairi kuichapa Iran, kuiwekea vikwazo kiuchumi

Donald Trump
Spread the love

NCHI ya Marekani imetangaza kuiwekea vikwazo vya kiuchumi vya kihistoria Iran, hadi pale taifa hilo litakapoacha kufadhili vikundi vya ugaidi pamoja na matumizi ya silaha za nyuklia. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa … (endelea).

Msimamo huo umetolewa leo tarehe 8 Januari 2020 (Januari 9, 2020 kwa majira ya Marekani), na Rais Donald Trump wakati akihutubia taifa hilo, kuhusu shambulio la makombora lililotekelezwa na Irani, kwenye kambi zake za jeshi zilizoko Iraq.

Trump amesema taifa lake lina vikosi vya jeshi vyenye nguvu na dhana bora za kivita , lakini haitatumia nguvu ya jeshi kukabiliana na Iran, isipokuwa itaiwekea vikwazo vya kiuchumi, ambavyo haijawahi kuwekewa.

Kiongozi huyo wa Marekani ametoa wito kwa mataifa yenye nguvu duniani, kuungana kwa pamoja ili kuidhibiti Iran, dhidi ya matumizi yake ya nyuklia pamoja na kufadhili vikundi vya ugaidi.

“Marekani ilivumilia sana uharibifu wa Iran, sasa siku za uvumilivu huo zimekwisha. Irani imekuwa ikiongoza kwa kufadhili vikundi vya ugaidi na matumizi ya nyuklia. Lakini katika uongozi wangu hilo halitatokea tena,” amesema Trump.

Kuhusu shambulio lililotokea jana nchini Iraq dhidi ya kambi zake za jeshi, Trump amesema hakuna mwanajeshi aliyepoteza maisha, lakini kuna majeruhi.

Trump amewaondoa wasiwasi Wamarekani akisema kwamba, hakuna uhai wa raia wa taifa hilo utakaopotezwa kutokana na mgogoro huo.

Kwa kuwa, vikosi vyake vya ulinzi na usalama vina mifumo thabiti, ya kulinda usalama wao pamoja na taifa lao.

Akizungumzia mauaji ya Jenerali Qasem Soleiman, aliyekuwa Kiongozi Mwandamizi wa Jeshi la Iran, Trump amesema jeshi lake lililazimika kumuua baada ya kubaini kupanga shambulio jipya dhidi ya Marekani.

“Soleiman aliongoza mashambulizi mengi dhidi ya Marekani, siku za hivi karibuni alipanga kutekeleza shambulio jipya dhidi yetu. Tukamdhibiti kwa kumuua. Mikono yake ilikuwa na damu ya Wamarekani na Wairan. Alitakiwa kudhibitiwa muda mrefu,” amesema Trump.

Trump amesema kifo cha Soleiman ni ujumbe tosha, kwa nchi zinazofadhili vikundi vya kigaidi na kuunga mkono matumizi ya silaha za nyuklia.

Hata hivyo, amesema Marekani haitegemei chochote kutoka kwa nchi zilizoko Mashariki ya Kati, kwa kuwa inajitosheleza kwa kila kitu.

Amesema kwa sasa Marekani inaongoza kwa  uzalishaji mafuta na gesi.

Mvutano baina ya Marekani na Iran uliibuaka kufuatia kifo cha Jenerali Soleiman, kilichotokea tarehe 3 Januari 2020 mjini Baghdad nchini Iraq.

Jeshi la Marekani lilimuua Jenerali Soleiman kupitia shambulio la anga.

Baada ya shambulio hilo, Iran ilijibu mapigo kwa kushambulia kambi za wanajeshi wa Marekani, zilizoko katika miji ya Irbil na Al Asad nchini Iraq.

Baada ya shambulio hilo kutokea nchini kwake, Iraq ilitangaza kuwafurusha wanajeshi wote wa kigeni walioko katika ardhi yake. Huku walengwa ikiwa ni wanajeshi wa Marekani.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

Kimataifa

Majaji kuamua hatima ya Zuma leo

Spread the loveMajaji nchini Afrika Kusini leo Jumanne wataamua ikiwa rais wa...

Habari za SiasaKimataifa

Spika Afrika Kusini ajiuzulu kwa tuhuma za rushwa

Spread the loveSpika wa Bunge la Afrika Kusini, Nosiviwe Mapisa-Nqakula ametangaza kujiuzulu...

Habari MchanganyikoKimataifa

Tetemeko la ardhi laua 7, lajeruhi 800 Taiwan

Spread the loveWatu wapatao saba wamefariki dunia na wengine zaidi ya 800...

error: Content is protected !!