June 30, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Marekani yadai kumuua aliyepanga kushambulia Kabul

Spread the love

 

JESHI la Marekani limesema, limemuua mtu anayedaiwa kupanga shambulizi kwenye uwanja wa ndege wa Kabul katika shambulizi la ndege isiyo na rubani. Inaripoti mitandao ya kimataifa…(endelea).

Shambulizi hilo la jana Ijumaa, tarehe 27 Agosti 2021, lilimlenga mtuhumiwa wa kundi la wanamgambo linalofungamana na linalojiita Dola la Kiislamu, IS-K kwenye jimbo la Nangahar, limefanyika baada ya Rais Joe Biden wa Marekani, kuapa kupambana na IS kufuatia shambulizi la juzi.

Aidha, Marekani imesema, itaendelea kuwaondoa raia wa Afghanistan kutoka uwanja wa ndege wa Kabul hadi dakika ya mwisho, licha ya kuwepo wasiwasi kuhusu mashambulizi kutoka kwa kundi la IS.

Wizara ya Ulinzi ya Marekani imesema bado kuna vitisho vya kuaminika katika uwanja huo wa ndege.

Marekani bado inaendelea na mchakato wa kuwaondoa raia wa Afghanistan wanaotaka kuondoka.

Msemaji wa kundi la Taliban amesema wamechukua udhibiti wa maeneo ya uwanja wa ndege. Hata hivyo, Marekani imekanusha taarifa hizo.

error: Content is protected !!