Saturday , 20 April 2024
Home Gazeti Habari Marekani yaanza kujiimarisha Afrika, kutoa Sh. 128.4 trilioni
HabariKimataifa

Marekani yaanza kujiimarisha Afrika, kutoa Sh. 128.4 trilioni

Joe Biden
Spread the love

 

RAIS wa Marekani Joe Biden ameahidi kuimarisha uhusiano na mataifa ya Afrika, huku akitangaza kusudio la Serikali yake kutoa kiasi cha Dola 55 bilioni (Sh. 128.4 trilioni), kwa ajili ya kusaidia bara hilo kwenye masuala ya chakula na mabadiliko ya tabia ya nchi. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa…(endelea).

Kwa mujibu wa mtandao wa Reuters, Rais Biden alitoa ahadi hiyo jana Jumatano, katika hafla ya chakula cha jioni na viongozi wa mataifa ya Afrika, iliyofanyika katika Ikulu ya White House.

Nao mtandao wa BBC Swahili, leo Alhamisi, umeripoti kwamba kiongozi huyo wa Marekani, ametangaza makubaliano yenye lengo la kuimarisha uhusiano wa kibiashara kati ya taifa lake na nchi za Afrika, uliodorora kufuatia China kuongeza ushawishi wake barani humo.

Biden alisema mkataba mpya na eneo la Biashara Huria la Bara la Afrika, utazipa kampuni za Kimarekani uwezo wa kufikia watu bilioni 1.3 na soko lenye thamani ya dola trilioni 3.4.

Mkutano wa wakuu wa nchi za Afrika na Serikali ya Marekani, unafanyika kwa siku tatu, kuanzia Jumanne hadi Alhamisi, ambapo marais mbalimbali wamehudhuria akiwemo Rais wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan. Rais wa Kenya, Dk. William Ruto. Rais wa Uganda, Yoweri Museveni na Rais wa Rwanda, Paul Kagame.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

Kimataifa

Majaji kuamua hatima ya Zuma leo

Spread the loveMajaji nchini Afrika Kusini leo Jumanne wataamua ikiwa rais wa...

Habari za SiasaKimataifa

Spika Afrika Kusini ajiuzulu kwa tuhuma za rushwa

Spread the loveSpika wa Bunge la Afrika Kusini, Nosiviwe Mapisa-Nqakula ametangaza kujiuzulu...

Habari MchanganyikoKimataifa

Tetemeko la ardhi laua 7, lajeruhi 800 Taiwan

Spread the loveWatu wapatao saba wamefariki dunia na wengine zaidi ya 800...

error: Content is protected !!