May 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Marekani, Uingereza zazungumzia mkutano wa Lissu na Samia

Spread the love

 

NCHI za Marekani na Uingereza, kupitia balozi zake nchini Tanzania, zimepongeza hatua ya Rais Samia Suluhu Hassan, kufanya mazungumzo na Makamu Mwenyekiti wa Chadema Bara, Tundu Lissu, jana tarehe 16 Februari 2022, jijini Brussels, Ubelgiji. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).

Pongezi hizo zimetolewa katika nyakati tofauti na Donald J. Wright (Balozi wa Marekani) na David Concar (Balozi wa Uingereza), katika akaunti zao za mtandao wa Twitter.

Katika akaunti yake hiyo, Balozi Wright amesema penye majadiliano hapaharibiki jambo.

“Hongera Rais Samia na Lissu kwa kuketi pamoja Ubelgiji, penye majadiliano hapaharibiki jambo,” ameandika Balozi Wright.

Naye Balozi Concar, jana kupitia kauanti yake ya Twitter naye aliipongeza hatua hiyo akisema inatia moyo kwa marafiki wa nchi kila kona.

“Hatua kama hizi zinahitaji nguvu na ujasiri. Marafiki wa Tanzania kila mahali watashangili. Hongera sana,” ameandika Concar.

Kwa mujibu wa Lissu, ameutumia mkutano wake na Rais Samia, kumfikishia masuala matano, ikiwemo kesi ya ugaidi inayomkabili Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na walinzi wake watatu, Halfan Bwire Hassan, Adam Kasekwa na Mohammed Abdilah Ling’wenya.

Kwenye Mahakama Kuu, Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi, jijini Dar es Salaam.

Mengine ni zuio la mikutano ya vyama vya siasa vya upinzani, mchakato wa upatikanaji katiba mpya na mfumo mpya wa uchaguzi utakaohakikisha uwepo wa chaguzi huru na za haki.

error: Content is protected !!