August 9, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Marekani, Uingereza kuchunguza kifo cha Musando wa Kenya

Chris Musando, aliyekuwa Kaimu Mkurugenzi wa Masuala Teknolojia wa Tume ya Uchaguzi na Mipaka Nchini Kenya (IEBC)

Spread the love

MAUAJI ya Kaimu Mkurugenzi wa Masuala Teknolojia wa Tume ya Uchaguzi na Mipaka Nchini Kenya (IEBC), yameziibua nchi za Marekani na Uingereza na kuamua kuungana na nchi hiyo kufanya uchunguzi wa kifo cha mtalaam huyo, anaandika Victoria Chance.

Chris Musando ambaye alikuwa msimamizi wa mifumo ya kompyuta ambayo ingesaidia kuzuia wizi wa kura wakati wa uchaguzi  mkuu unaotarajia kufanyika mwezi huu, aliuawa jumamosi iliyopita nchini humo.

Polisi wameeleza kuwa mwili wa Musando pamoja na mwanamke ambaye hakutambulika ulipatikana jijini  Nairobi, eneo la Kikuyu.

Gazeti la Daily Nation limeripoti kuwa Mabalozi wa Marekani nchini  Kenya, Robert Godec na Nic Hailey, wa Uingereza wamelaani mauaji hayo na kuongeza kuwa watashiriki katika uchunguzi huo.

error: Content is protected !!