Rex Tellerson, Waziri wa Mambo ya Kigeni Nchini Marekani amejibu juu ya jaribio la pili la kombora la masafa marefu lililofanywa na Korea Kaskazini, anaandika Irene Emmanuel.
“Sisi si maadui zenu, sisi si tisho kwenu , lakini mnatuwekea tisho lisilo kubalikana lazima tujibu.” Amesema Tellerson.
ameyasema hayo baada ya Korea Kaskazini kufanya jaribio la pili la kombora la masafa marefu linalojulikana kama Inter-continental Ballistic Missile (ICBM), tar 28 julai linaloweza kushambulia bara jingine.
“Hatutaki mabadiliko ya utawala, hatulengi kuuangusha utawala, hatutaki kuharakisha muungano wa eneo la Peninsula, hatutaki sababu ya kutuma wanajeshi wetu kwenye eneo lenu.” Amesema Tillerson, akimaanisha mpaka baina ya Korea kaskazini na Korea Kusini.
Ikumbukwe kuwa Donald Trump, Rais wa Marekani aliwahi kumwambia Seneta wa Chama cha Republican kuwa kunaweza kuwa na vita dhidi ya Korea Kaskazini kama mpango wao wa makombora utaendelea.
Leave a comment