September 23, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Marekani kutoa dola 100 kwa atakayekubali chanjo ya Korona

Joe Biden, Rais wa Marekani

Spread the love

 

RAIS wa Marekani, Joe Biden ameanzisha utaratibu wa kutoa dola 100 (Sh.231900), kwa kila mwananchi atakaye kubali kuchanjwa chanjo ya Ugonjwa wa Korona, ikiwa ni jitihada za kutokomeza maambukizi ya wimbi la tatu la janga hilo, nchini humo. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa … (endelea).

Biden ametangaza uamuzi huo jana tarehe 29 Julai 2021, akilihutubia Taifa hilo akiwa Ikulu ya White House, Marekani.

Rais huyo wa Marekani, aliagiza maafisa wa Serikali za mitaa nchini humo, kutoa fedha hizo kama motisha kwa watu watakaokubali chanjo hiyo.

Rais Biden alisema kuwa, uamuzi huo utawafanya wananchi wa Marekani, kuwa na mwamko wa kupata chanjo kuliko kutumia nguvu.

Pia, Rais Biden aliagiza watumishi wa Marekani, kutoa vielelezo vinavyoonesha kama wamepata chanjo ya Korona.

error: Content is protected !!