September 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Marekani, JPM waungana kuelekea uchaguzi mkuu 2020

Rais John Magufuli, Mwenyekiti wa Jumuiya ya SADC akihutubia wajumbe wa mkutano huo

Spread the love

AHADI ya Rais John Magufuli kwamba, atahakikisha uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka huu unakuwa huru na haki, imeungwa mkono na Marekani. Anaripoti Martin Kamote, Dar es Salaam…(endelea).

Taarifa ya Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania iliyotolewa leo tarehe 31 Januari 2020, imeeleza kufurahishwa na ahadi ya Rais Magufuli aliyoitoa tarehe 21 Januari 2020 kwamba, uchaguzi huo hautafinyangwa.

“Mwaka 2020 mwezi Oktoba, nchi yetu itafanya uchaguzi mkuu, zoezi la uchaguzi ni muhimu kwa nchi yoyote inayofuata misingi demokrasia, Serikali imejipanga kuhakikisha kuwa uchaguzi mkuu unafanyika katika mazingira ya amani, uhuru na haki” alisema Rais Magufuli.

Alitoa kauli hiyo alipokutana na mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao  Tanzania wenye sherehe za mwaka mpya 2020 na chakula cha jioni Ikulu, Dar es Salaam.

Taarifa ya ubalozi huo imeeleza “tumetiwa moyo sana na hakikisho lililotolewa na Raisi Magufuli hapo tarehe 21 Januari 2020, kwamba uchaguzi mkuu wa mwaka 2020, utakuwa huru, haki na uwazi pamoja na mwaliko wake kwa waangalizi wa uchaguzi wa kimataifa.

“Tunatarajia uchaguzi ambao raia wote na wagombea wa vyama vyote, wanaweza kukutana kwa amani, wakieleza mawazo yao na kampeni zitakazofanyika katika misingi ya usawa.”

Hata hivyo, Ubalozi umetoa wito kuhakikishiwa zoezi la uandikishaji wapiga kura lenye uwazi, kuanzishwa kwa Tume Huru ya Uchaguzi na kuteuliwa mapema kwa waangalizi wa uchaguzi wa kitaifa na kimataifa wa kuaminika, na watakaofuatilia uchaguzi kwa kipindi kirefu na kifupi.

error: Content is protected !!