August 18, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Marekani iliifanya Cuba danguro

Fidel Castro, Mwanamapinduzi nchini Cuba

Spread the love

SANTIAGO  ndio mji ambao amezikwa mwanamapinduzi Fidel Castro Ruz nchini Cuba. Mji huu upo Kusini, Mashariki mwa kisiwa hicho kikubwa kupita vyote katika ukanda wa Bahari ya Caribbean, anaandika Wolfram Mwalongo.

Majivu ya mwanamapinduzi huyo yamezikwa tarehe 4 Desemba wiki iliyopita. Simanzi na vilio ndivyo vilivyotawala kwa Wanacuba wakati wa maziko hayo.

Hii inaonesha wazi namna walivyothamini na kuheshimu mchango wa mwanamapinduzi huyo katika maisha yake ndani ya kisiwa hicho.

Kifo cha Castro kilitangazwa Novemba 25 mwezi uliopita na rais wa sasa Raul Castro ambaye ni mdogo wake.

Raul alitangaza utaratibu utakaofuatwa na raia wote katika kipindi hicho kigumu wakati wa maombolezo ya siku nane huku bendera zikipepea nusu mlingoti kama ishara ya heshima kwa kuondokewa na kiongozi mkubwa wa taifa hilo.

Taarifa za msiba huo zilishtua wengi, hususan mataifa yaliyoafiki msimamo wa mwanamapinduzi wa kikomunisti ikiwemo Afrika kutokana na mchango wake mkubwa.

Angola, Namibia Afrika Kusini ni miongoni mwa mataifa ambayo yalipata kusaidiwa na Jeshi la Cuba katika harakati zake za kujipatia Uhuru.

Msiba wa shujaa huyo aliyetikisa Karne 19 kupinga tawala za kidhalimu ikiwemo Marekani, taifa ambalo limekoseshwa uzingizi kwa miaka 32, miaka aliyongoza Fidel Cuba kama rais.

Marekani ilifanya kisiwa hicho kuwa danguro lake kutokana Dikteta  Flugencio Batista, aliyekuwa Rais wa Cuba kuzama kwenye mahaba ya gafla na Marekani.

Alikuwa tayari kulamba nyayo za Marekani kutokana na msaada aliokuwa akiupata kutoka kwenye taifa hilo. Aliongoza taifa hilo kuanzia mwaka 1952 hadi 1959 kwa kutumia mabavu kutokana na kuungwa mkono na Marekani.

Ardhi ya Cuba iliyohodhiwa na Kampuni za Marekani ilitaifishwa na Castro ambaye aliitazama Marekani katika sura mbili; ya kibeberu na unyonyaji kitendo kichopelekea taifa hilo kuvunja mahusiano na Cuba.

Utawala wa Castro nchini Cuba uliiweka Marekani roho juu kutokana na yeye kujiunga na nchi za Umoja wa Kisovieti, aliitaka Urusi kutengeneza silaha za nyuklia kwenye kisiwa cha Cuba.

Hofu ya Marekani kwa Cuba ilikuwa ni uzalishaji wa silaha za nyuklia kutokana na ukaribu uliopo baina ya mataifa hayo mawili. John Kennedy, Rais wa 35 wa Marekani alitangaza kuiwekea vikwazo nchi ya Cuba.

Wachambuzi wa maswala ya kisiasa walikuwa wakikosoa dhana iliyojengeka na inayoendeleea kupotosha ukweli juu ya vinavyoitwa vikwazo vya Marekani kwa Cuba.

Wachambauzi wengi wanasema Cuba ilikuwa huru kwa kuwa iliweza kutoa elimu na kuweza kusaidi mataifa mwengine kupata uhuru.

Wapo wanaotazama kwamba Marekani ndio iliyowekewa vikwazo, hilo linadhilishwa na nama ambavyo Rais Kennedy alivyohaha kuushawishi Umoja wa Mataifa (UN) kuiwekea vikwazo taifa hilo.

Hivi sasa Marekani imepata ahueni, ni baada ya kukata pumzi ya mwanamapinduzi na muasisi wa ukomunisti nchi  Cuba. Marekani inaamini kurejesha uhusiano wake na Cuba uliopotea kwa miaka zaidi ya 50 sasa.

Ingawa miezi miwili kabla ya kifo chake alisema wazi kwamba, hakubaliani na mwenendo wa Marekani kutokana  kuwa kikwazo kwa maendeleo ya mataifa mengi duniani hususan yanayokubari kulamba nyayo za taifa hilo.

error: Content is protected !!