Tuesday , 3 October 2023
Home Kitengo Habari Kimataifa Marekani, China washusha uchumi wa Dunia
KimataifaTangulizi

Marekani, China washusha uchumi wa Dunia

Dola za Marekani
Spread the love

MIVUTANO ya kibiashara ya kidunia imetajwa kuwa miongoni mwa sababu za kushuka kwa uchumi  wa dunia katika kipindi cha mwaka 2018/2019 huku vita ya kibiashara baina ya nchi ya Marekani na China ikihatarisha kuvurugika kwa mwenendo wa biashara za kimataifa. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea)

Kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa leo na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) kufuatia utafiti wake wa hivi karibuni  inaeleza kuwa, hatua ya Marekani kutangaza viwango vipya vya ushuru pamoja na madeni makubwa, pia imeshusha uchumi wa dunia.

Mchumi Mkuu wa IMF, Maury Obstefeld akizungumzia kuhusu hali ya uchumi duniani, amesema ukuaji wa uchumi wa dunia kwa mwaka 2018/2019 utasalia katika kiwango cha asilimia 3.7 ambacho ni kiwango pungufu ukilinganisha na asilimia 3.9 kiwango kilichotangazwa mwezi Aprili mwaka huu.

Ripoti ya IMF vile vile imebainisha  kwamba, kiwango cha kukua kwa uchumi wa mataifa yenye uchumi mkubwa duniani, China na Marekani pia kimeshuka.

Ambapo China inatabiriwa uchumi wake kushuka kwa asilimia moja kutoka asilimia 6.4 ilivyo sasa hadi asilimia 6.2 ifikapo mwaka 2019.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Serikali kupokea ndege ya 14 ya ATCL, safari kuongezeka

Spread the love  SERIKALI ya Tanzania, kesho tarehe 3 Oktoba 2023, inatarajia...

Habari MchanganyikoTangulizi

Mobhare Matinyi Msemaji mpya wa Serikali

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amemteua aliyekuwa Mkuu wa...

Kimataifa

Urusi yafungua milango kwa nchi za Afrika

Spread the loveSERIKALI ya Urusi imefungua milango ya ushirikiano wa kiuchumi, kijamii...

Habari MchanganyikoTangulizi

Basi la Magereza lagonga treni yenye abiria 650 Dar

Spread the loveBasi  Jeshi la Magereza lenye namba MT 0040 limegonga treni...

error: Content is protected !!