January 23, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Marando: UKAWA ni imara

Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mabere Marando

Spread the love

MABERE Marando, Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) amesema, Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) upo imara. Anaandika Pendo Omary … (endelea).

Marando ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kanda ya Pwani wa chama hicho, ametoa kauli hiyo kufuatia kuwepo kwa taarifa kwamba, kitendo cha Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Prof. Ibrahim Lipumba kuchukua fomu na kutangaza nia ya kuutaka urais ni dalili ya kuparanganyika kwa UKAWA.

Marando ametoa msimamo huo jana jijini Dar es Salaam wakati wa akizindua “Operasheni Amsha Wanawake Tanzania” iliyoandaliwa na kada wa Chadema pia Mkurugenzi wa bendi ya wanawake, Lilian Wasira kwa ushirikiano na Baraza la Wanawake wa Chadema (BAWACHA).

“Profesa Lipumba kuchukua fomu ya urais ni utaratibu wa kawaida ambao viongozi wa UKAWA wamekubaliana. Lazima kila chama kifuate utaratibu, kwa mujibu wa chama hicho. Hata kwa Chadema itakuwa hivyo hivyo,” amesema Marando.

Aidha, Mabere ameongeza kuwa “UKAWA tupo imara. Hatujatetereka. Tutawapa Watanzania mgombea mmoja wa kiti cha urais, mgombea mmoja kila jimbo na mgombea mmoja wa kiti cha udiwani.”

Pia Marando ameahidi kuwapo viongozi wake kura milioni tatu za wananchi wa mikoa ya Dar es Salaam na Pwani.

Kwa upande wake, Lilian amesema lengo la opereshini hiyo ni kutumia bendi ya wanawake kuwaamsha na kuwajengea wanawake uwezo nchi nzima ili wajitambue na kudai haki zao.

“CCM imetufanya kama yatima. Hata haya mauaji ya albino yasingekuwepo kama tungekuwa na viongozi bora. Tutaenda katika kila kona ya nchi kuwaamsha wanawake waweze kujiandikisha na kuchagua viongozi bora kutoka UKAWA,” amesema Lilian.

Aidha Jesca Kishoa Kafulila ambaye amejipanga kumng’oa Mwigulu Chemba katika Jimbo la Iramba Magharibi amesema “asilimia 60 – 65 ya wapiga kura nchini ni wanawakehivyo uzinduzi wa oparasheni hii ni ujumbe tosha kwa CCM, kwamba Oktoba 25 wajiandae kuondoka madarakani.”
error: Content is protected !!