Sunday , 3 December 2023
Home Kitengo Habari Kimataifa Marais wastaafu Marekani wamsulubu Trump
Kimataifa

Marais wastaafu Marekani wamsulubu Trump

Donald Trump, Rais wa Marekani
Spread the love

MARAIS wastaafu wa Marekani, Bill Clinton na Jimmy Carter wamesema Donald Trump, rais wa sasa wa Taifa hilo amesababisa vurugu kwa taifa hilo. Inaripoti mitandao ya kimataifa … (endelea).

Wametoa kauli hiyo baada ya Joel Biden kuidhinishwa rasmi na Chama cha Democratic kuwania urais kupitia chama hicho, kwenye uchaguzi mkuu utakaofanyika Novemba 2020.

Clinton aliyeongoza Marekani kuanzia 1993-2001, kwenye hotuba yake usiku wa kuamkia leo Jumatano tarehe 19 Agosti 2020, amesema Marekani ndio nchi iliyopiga hatua kubwa kiuchumi duniani lakini watu waliokosa ajira wameongezeka mara tatu zaidi katika uongozi wa Trump.

Amesema, utawala wa Trump umeshindwa kutatua changamoto ya ajira pamoja na tatizo la janga la corona kutokana na mbinu zisizokuwa na makali kutumika.

Carter aliyeongoza taifa hilo kuanzia Januari 1977 – Januari 1981 ameeleza kushangazwa na Trump katika kukabiliana na mihemuko ya Wamarekani huku akigusia uhusiano wa Marekani na nchi za nchi ulivyoyumba.

Wastaafu wote kwa pamoja, wameeleza kumuunga mkono Biden kutokana na kile walichoita historia yake na uwajibikaji wake katika maeneo mbalimbali aliyopita.

Carter amewataka Wamarekani kutofanya kosa, kwa kuwa nafasi ya kufanya marekebisho imebaki moja nayo ni kwenye uchaguzi mkuu ujao.

Colin Powell, Waziri wa Wambo ya Nje mstaafu na mwanachama wa Chama cha Republican amemtaja Biden kwamba, ni mtu mwenye maadili aliyojifunza wakati mwanajeshi na kwamba anamuunga mkono ili arejeshe maadili katika Ikulu ya nchi hiyo.

Powell, aliyehudumu nafasi hiyo wakati wa utawala wa Rais George W. Bush, anamtaja Trump kama kiongozi muongo.

Waziri huyo mstaafu anaungana na wanachama wengine wa Republican ambao wameridhishwa na uamuzi wa Democratic kumuidhinisha Biden kuwa mgombea urais.

Mwanachama mwingine maarufu wa Republican anayemuunga mkono mgombea wa Democratic ni aliyekuwa gavana wa Ohio, John Kasich.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Kimataifa

Muandamanaji ajichoma moto akipinga vita Palestina, Israel

Spread the loveMUANDAMANAJI moja ambaye hajafahamika jina, yuko mahututi hospitalini akitetea uhai...

Kimataifa

Urusi kuongeza wanajeshi ikijihami dhidi ya NATO

Spread the loveSERIKALI ya Urusi iko katika mpango wa kuongeza wanajeshi wake,...

Kimataifa

Israel yarejesha mashambulizi Gaza ikilaumu Hamas kukiuka makubaliano

Spread the loveJESHI la Israel, limerejesha mashambulizi katika ukanda wa Gaza, baada...

Kimataifa

Papa Francis kumfukuza Kardinali anayepinga mageuzi Kanisa Katoliki

Spread the loveKIONGOZI wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Francis, anadaiwa kupanga kumfumkuza...

error: Content is protected !!