Friday , 29 March 2024
Home Habari Mchanganyiko Mapya yaibuka sakata la ndoa ya mbunge CCM
Habari MchanganyikoTangulizi

Mapya yaibuka sakata la ndoa ya mbunge CCM

Spread the love

 

MWANAMKE anayedai kuwa ni mchumba, aliyezaa na kuishi na mbunge wa Korogwe Vijijini (CCM), Timotheo Mnzava, anamtuhumu Mchungaji wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, Usharika wa Meru, mkoani Arusha, “kushiriki usaliti wa mchumba wake.” Anaripoti Hamisi Mguta, Dar es Salaam … (endelea).

Mchungaji huyo anayejulikana kwa majina ya Franael Joshua Issangya, anatuhumiwa kuchangia kwa kiwango kikubwa, Mzava kutelekeza familia yake na kutafuta mwanamke mwingine wa kufunga naye ndoa.

Mnzava yuko mbioni kufunga ndoa na Caroline Pallangyo, ambaye ni mtoto wa mbunge wa Arumeru Mashariki (CCM), John Pallangyo.

Ndoa kati ya Mzava na mtoto wa mbunge mwenzake, inatarajiwa kufungwa katika KKKT, Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, Usharika wa Mombo, mkoani Tanga, tarehe 10 Julai 2021.

Undani wa nini kimeibuka upya, majibu ya mchungaji huyo anayetuhumiwa na mengine yanayoendelea, soma Gazeti la Raia Mwema, toleo la leo Jumamosi, tarehe 3 Julai 2021.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

Habari za SiasaTangulizi

Mashirika matano yapata hasara mabilioni ya fedha

Spread the loveMASHIRIKA matano ya Serikali yanayojiendesha kibiashara, yamepata hasara ya mabilioni...

Habari Mchanganyiko

Mtandao watetezi wa haki za mazingira Tanzania waundwa

Spread the loveMTANDAO wa watetezi wa haki za mazingira nchini Tanzania, umeundwa...

error: Content is protected !!