Spread the love

 

SIRI dhidi ya mauaji ya mfanyabiashara wa madini, Mussa Khamisi, maarufu “Mussa Dola,” anayedaiwa kuporwa kiasi cha Sh.70 milioni na kisha kuuawa kwa kuchomwa sindano ya sumu na polisi mkoani Mtwara na baadae mwili wake kuutupa baharini, zinadizi kufichuka. Anaripoti Mwandishi Wetu, Mtwara … (endelea).

Taarifa mikononi mwa gazeti la Raia Mwema la leo Jumatano tarehe 26 Januari 2022, zinasema, mbali na maofisa wa polisi kutuhumiwa kufanya mauaji hayo ya kinyama na kupora fedha hizo, walikwapua kutoka kwa mama wa marehemu, Hawa Bakari Ally kiasi kingine cha Sh. 3.2 milioni.

Fedha hizo zilizokutwa nyumbani kwa wazazi wa mtuhumiwa zilikuwa michango ya Vikoba, iliyohifadhiwa na mama wa Mussa.

Tayari maofisa saba wa polisi wamefikishwa mahakamani mkoani Mtwara kwa tuhuma za mauaji ya mfanyabiashara huyo, mkazi wa Kijiji cha Ruponda wilayani Nachingwea, mkoani Lindi.

Mauaji hayo yalifanyika tarehe 5 Januari 2022 na mwili wa marehemu ukatupwa kitongoji cha Majengo kijiji cha Hiari, wilayani Mtwara.

Maafisa wa Polisi waliofikishwa mahakamani, ni Mrakibu wa Polisi Gilbert Kalanje; Mkuu wa Upelelezi wa wilaya ya Mtwara, Mrakibu Msaidizi wa Polisi Charles Onyango na Mrakibu wa Polisi Msaidizi, Nicholaus Kisinza.

Wengine, ni Mkuu wa Kikosi cha Intelejensia ya Jinai mkoa wa Mtwara, Mkaguzi wa Polisi, John Msuya Mganga; Mkuu wa Zahanati ya Polisi Mtwara, Mkaguzi wa Polisi Msaidizi, Marco Mbuta, Mkaguzi wa Polisi, Shirazi Mkupa na Koplo Salimu Juma Mbalu.

Afisa mwingine wa Polisi, Inspekta Msaidizi wa Polisi, Grayson Gaitan Mahembe, anadaiwa kujinyonga Januari 22 mwaka huu, akiwa mahabusu ya Polisi, mkoani Mtwara.

Kwa habari zaidi soma Raia Mwema la leo…

One Response

  1. Hii ndiyo sura halisi ya POLISI wa nchi hii. NI aibu kubwa kwa waziri kuwa na watumishi wa aina hii. Viongozi wakuu wawajibike kwa hili au wafukuzwe kazi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *