June 17, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Mapya yaibuka hukumu ya Katumbi

Spread the love

HUKUMU ya kifungo cha miaka mitatu kwa Moise Katumbi Kiongozi wa Upinzani na rais wa klabu ya soka ya TP Mazembe ya nchini Kongo ilitolewa kwa shinikizo la Majasusi na wakuu wa mahakama, anaandika Wolframa Mwalongo.

Chantal Ramazani mmoja wa majaji waliosikiliza kesi hiyo ambaye kwa sasa yupo uhamishoni amekiri kwamba lengo lilikua ni kumzuia kiongozi huyo kugombea nafasi ya urais katika uchaguzi unaotarajia kufanyika mwaka huu nchini Kongo.

Katika hukumu iliyotolewa 23 Juni mwaka huu mjini Kamalondo- Lubumbashi, Katumbi anadaiwa kuuza mali kinyume na sheria za nchi hiyo.

Hata hivyo wakati kesi hiyo ikiendeshwa kiongozi huyo wa upinzani alikuwa nchini Afrika ya Kusini kwa matibabu, ambapo mpaka sasa bado hajarejea nchini Kongo.

Aidha Uchaguzi mkuu nchini humo unatarajiwa kufanyika mwezi Novemba mwaka huu huku kukiwa na mvutano baina ya Rais Joseph Kabila na vyama vya upinzani.

Rais Kabila anatakiwa kuachia ngazi wakati huu kwa mujibu wa katiba ya nchi hiyo lakini wapinzani wake wanadai anapanga njama ya kuendelea kubakia madarakani kinyume na katiba.

Taarifa zaidi zinaeleza kuwa, Katumbi anatarajia kurudi nchini humo mwishoni mwa juma hili baada ya kuimarika kwa afya yake.

error: Content is protected !!