May 26, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mapokezi ya Simba yasimamisha Kigoma

Spread the love

KIKOSI cha klabu ya Simba, kimewasili mkoani Kigoma kwa ajili ya mchezo wa Fainali wa kombe la Shirikisho dhidi ya Yanga. Anaripoti Kelvin Mwaipungu…(endelea)

Mchezo huo utapigwa siku ya Jumapili, tarehe 25 julai 2021, kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika, mkoani humo.

Kikosi cha Simba kiliwasili Kigoma, majira ya saa 12:13 jioni kwa shirika la ndege la Air Tanzania na kupokelewa na mashabiki wao waliojitokeza Uwanjani hapo.

Simba ilianza safari ya kuondoka Uwanjani hapo majira ya saa 12:25 wakiwa na msululu wa mashabiki na kuelekea katikati ya mji.

Kikosi hiko kilitumia Saa 1 kufika kwenye hotel ya Tanganyika ambapo kambi ya timu hiyo ilipo.

Msafara wa Simba uliongozwa na mtendaji Mkuu wa klabu hiyo Barbara Gonzalez, na baadhi ya viongozi wengine waandamizi wa timu hiyo.

Mara baada ya kuwasili Kigoma, kikosi hiko kesho asubuhi kitafanya mazoezi kwa mara ya kwanza kwenye Uwanja wa Chuo cha Hali ya Hewa.

Yanga ilikuwa ya kwanza kutumia Uwanja juo siku ya jana, katika mazoezi yao ya jionii, na leo klabu ya Simba itafanya pia mazoezi kwenye Uwanja huo huo.

Mara ya mwisho timu hizo zilikutana Julai 3 Mwaka huu kwenye mchezo wa Ligi Kuu soka Tanzania Bara, na Simba kupoteza mchezo huo kwa bao 1-0.

 

error: Content is protected !!