May 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mapinduzi arejea uwanjani Yanga ikiibuka na ushindi

Spread the love

 

KLABU ya Soka ya Yanga imeibuka na ushindi wa mabao 2-0, kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya Mbuni FC ya mkoani Arusha huku tukushuhudia kurejea kiwanjani kwa kiungo mshambuliaji wa klabu ya Yanga Mapinduzi Balama ambaye alikaa nje kwa msimu mzima kutokana na kusumbuliwa na majeruhi. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea)

Mchezo huo wa kirafiki ulipigwa hii leo tarehe 19 Januari, 2022 jijini Arusha kwenye dimba la Sheikh Amri Abeid ambapo Yanga ipo mkoani humo kujiandaa na mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Polisi Tanzania.

Mchezo huo wa Ligi Kuu Tanzania Bara utapigwa siku ya Jumapili, tarehe 23 Januari 2022, kwenye dimba hilo hilo ambapo Polisi Tanzania atakuwa mwenyeji wa mchezo huo.

Mapinduzi anarejea kiwanjani kwa kupata dakika nyingi za kucheza toka alipopata maejeruhi ya kuvunjika kifundo cha mguu kwenye mzunguko wa pili msimu wa 2019/20 na kumuweka nje kwa msimu mzima.

Mara baada ya kupata majeruhi hayo Balama alisafirishwa na klabu hiyo kuelekea nchini Afrika Kusini kwa ajili ya kupata matibabu Zaidi kwa kufanyiwa tena upasuaji kisha kurejea nchini.

Kwenye mchezo huo wa kirafiki Balama alicheza dakika 45 za kipindi cha pili, mara baada ya kuingia akichukua nafasi ya Heritier Makambo.

Mabao ya Yanga kwenye mchezo huo yaliwekwa kambani na Tonombe Mukoko kwa njia ya mikwaju ya Penati.

error: Content is protected !!