Sunday , 19 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Mapigano kugombea ardhi, Serengeti, Butiama yanukia.
Habari MchanganyikoTangulizi

Mapigano kugombea ardhi, Serengeti, Butiama yanukia.

Spread the love

MAPIGANO ya kugombea ardhi ya kilimo na kufuga yanayohusisha silaha za jadi pamoja na bunduki yanatarajia kuendelea kutokea muda wowote katika kijiji cha Remung’orori na  Mikomariro mkoani Mara, anaripoti Mwandishi Wetu … )Endelea).

Wiki iliyopita  wananchi wa kijiji cha Mikomariro wilaya ya Butiama walivamia wakazi wa kijiji cha Remung;orori wilaya ya Serengeti na  kuua watu wawili kwa kutumia panga na shoka.

Kwa mujibu wa mwenyekiti wa kijiji cha Remung’orori, Msamba Maro, mauaji hayo yalitokea Ijumaa iliyopita wakati wananchi wake walipokuwa shambani.

Alisema wananchi hao wakiwa shambani walivamiwa na kundi kubwa la watu kutoka kijiji jirani cha Mikomariro na kuanza kuwakimbiza na kufanikiwa kumuua Wigesa Gikene kwa kumcharanga na panga.

Aliongeza kuwa mkazi mwingine ambaye anatoka kijiji cha Kenyamonta ambaye alikuwa shambani alipigwa shoka kichwani na kupoteza maisha na kundi hilo.

Maro alisema kwa muda mrefu kumekuwapo vita ya maneno kwa wakazi wa vijiji hivyo wakigombea eneo la Metoha na Motiribhe ambalo lipo kijiji cha Remungorori kwa mujibu wa mipaka ya vijiji iliyowekwa mwaka 1974.

Hata hivyo,  amesema wakazi wa kijiji cha Mikomariro kwa muda mrefu wamekuwa wakikaidi na kuvuka mipaka yao na kuingia upande wa pili na kujenga nyumba za kuishi na kuendesha shughuli za kilimo pamoja na ufugaji wa makundi makubwa ng’ombe.

Kwa mujibu wa  mkazi wa kijiji cha Remungorori, Mohamed George, uvamizi huo umezua hofu kutokana na kufanyika mauaji hayo ya kinyama.

George amesema siku ya tukio wananchi  wenzake walikuwa eneo la mashamba na ghafla wakatokea wavamizi na kuanza kuwakimbiza na kwa bahati mbaya waliwakamata watu wawili na kuwaua.

Alisema  mgogoro huo umekuwapo muda mrefu, lakini viongozi wa wilaya, mkoa hawajawahi kuchukua hatua ili kuumaliza.

Mkuu wa mkoa wa Mara,  Adam Malima akizungumza na wananchi wa kijiji cha Remung’orori,  wakati wa mazishi ya Gikene,  alitoa wito kwa wananchi hao kuwa na utulivu wakati serikali inatafuta njia ya kumaliza mgogoro huo.

Alikiri kwamba umefanyika uonevu kwa wananchi wa kijiji cha Remung’ororori, lakini akawataka wananchi hao kutolipiza kisasi.

Alikiri kwamba mgogoro huo umekuwapo siku nyingi huku chanzo kikuu kikiwa na wananchi wa kijiji cha Mikomariro kuvamia na kufanya mauaji.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

CCM yamteua Pele kuwa mgombea ubunge Kwahani

Spread the loveKamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Canada yatenga bilioni 38 kutekeleza mradi ya kuinua vijana TZ

Spread the loveSERIKALI ya Canada kupitia ‘CARE International Canada’ imetenga takribani Sh...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Ujenzi kituo cha kupoza umeme Chalinze wafikia asilimia 93.7

Spread the loveKamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini imeeleza...

Habari Mchanganyiko

Balile ateuliwa rais wa wahariri Afrika Mashariki

Spread the loveJumuiya ya Wahariri wa Afrika Mashariki (EAES), imemchagua Mwenyekiti wa...

error: Content is protected !!