Monday , 30 January 2023
Home Gazeti Habari Mchanganyiko Mapadre Mchamungu, Msomba wawekwa wakfu uaskofu Dar
Habari Mchanganyiko

Mapadre Mchamungu, Msomba wawekwa wakfu uaskofu Dar

Spread the love

 

MAPADRE Stephano Msomba na Henry Mchamungu wamewekwa wakfu wa kuwa maaskofu wasaidizi wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam nchini Tanzania. Anaripoti Noela Shila, TUDARCo … (endelea).

Maaskofu hao, wamewekwa leo Jumanne, tarehe 21 Septemba 2021 na Askofu Mkuu Mwandamizi wa Jimbo Kuu Katoliki Dar es Salaam, Jude Thadeus Ruwa’ichi.

Misa hiyo takatifu imefanyikia viwanja wa Msimbazi Center na kuhudhuriwa na maaskofu, mapadre, viongozi wa serikali na kisiasa, waumini na viongozi wa madhehebu ya dini wakiwemo Waislamu.

Mara baada ya kuwaweka wakfu, Askofu Mkuu Ruwa’ichi amesema “uaskofu ni utume, siyo heshima na cheo na wapendwa wetu, tunaowapongeza na kuwaombea leo, wanaingia katika kazi moja kwa moja.”

“Wanaanza kazi wote wawili na wanawajibika kama naibu maaskofu wa jimbo lote. Lakini tunao umuhimu wa kushirikishana kwa kulenga maeneo mbalimbali,” amesema

Askofu Mkuu Ruwa’ichi amesema, ili kuleta ufanisi zaidi, watagawana maeneo ambapo Askofu Mchangmu atahudumia Dekania za Mtakatifu Petro, Kilimahewa, Mbagala, na Makuburi.

Askofu Msomba atahudumia Dekani za mtakatifu, Josefu, Ukonga, Segerea na Kigamboni huku Askofu Mkuu Ruwa’ichi atahudumu dekania za Kibaha, Gasper, Mbezi Louis na Ubungo.

Askofu Mkuu Ruwa’ichi amezigawa Idara za Kurugenzi za Jimbo ambapo Askofu Mchamungu atahusika na masuala ya sheria, afya, mahakama ya kanisa, vijana, haki na amani na miito.

Askofu Msomba atahusika na vyama vya kitume, liturujia, ardhi, Uwaka, mawasiliano, katakesi, elimu na familia.

Yeye Askofu Mkuu Ruwa’ichi atahusika na uhungaji, mapadre, fedha, watawa, utoto mtakatifu, mahusiano mbalimbali na wawata.

Awali, wakizungumza na hadhira iliyohudhuria misa hiyo, Askofu Muchamungu amewaomba maaskofu kuwapokea katika kundi lao kwani wamewawekea mikono “naomba watusaidie ili tuweze kufanya kazi vizuri kama wao na sisi tuko tayari kushirikiana nao kama wachungaji wa kanisa.”

“Nawaomba mapadre ushirikiano wenu katika majukumu yao, kazi ya askofu inaweza kuwa rahisi sana kama kutakuwa na ushirikiano ili kazi yangu ya askofu niweze kuifanya vyema,” amesema.

Yuda Thadei Rwaichi, Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam

“Watawa na walei ninyi ni muhimu. Naomba sala zenu ili niweze kuishi kiapo cha uaminifu ambacho nimekiweka. Naombeni sala zenu na niweze kutekeleza majukumu ambayo nimekabidhiwa ya kufundisha, kutakatifuza na kuongoza,” amesema Askofu Muchamungu aliyekuwa mwalimu wa Seminari kuu, Segerea, Dar es Salaam

Kwa upande wake, Askofu Msomba amesea, “haikuwa rahisi wazazi wangu kuniruhusu kuwa mtawa, haikuwa rahisi sana kwani kulifanyika vikao vingi lakini mwisho wa siku wakaniruhusu. Nawaombea pumziko la milele huko walipo kwani wote wamefariki.”

“Kama alivyoongea pacha wangu, yeye ni kulwa na mimi ni doto. Tunawashukuru nyote akiwemo Askofu Ribena kwa kutuandaa hadi kuifikia siku hii ya leo. Nawashukuru wanafunzi wenzangu kuanzia shule za msingi na sekondari ya Maua.”

Askofu Msomba aliyekuwa Paroko wa Parokia ya Mavurunza amesema “tunakwenda kazini, si kazi ya siasa ni kazi ya utumishi. Tunaomba mtuombee na tusaidiane ili tuweze kufika mbinguni.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chongolo asikitishwa na mradi wa Mil 900 kutoanza kutoa manufaa

Spread the loveKATIBU mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa Daniel Chongolo...

Habari Mchanganyiko

Huawei Tanzania yatajwa miongoni mwa waajiri bora kimataifa

Spread the loveKAMPUNI ya Huawei Tanzania imetajwa kuwa mwajiri bora nchini na...

Habari Mchanganyiko

Waziri wa uchumi wa Finland atua nchini, kuteta na mawaziri 7

Spread the loveWAZIRI wa Masuala ya Uchumi wa Finland, Mika Tapani Lintilä...

Habari Mchanganyiko

Asimilia 79 wafeli somo la hesabu matokeo kidato cha nne

Spread the loveWATAHINIWA wa shule 415,844 sawa na asilimia 79.92 ya watahiniwa...

error: Content is protected !!