Wednesday , 8 February 2023
Home Gazeti Habari Mchanganyiko Mapacha waoa mwanamke mmoja… wanatarajia kupata mtoto
Habari Mchanganyiko

Mapacha waoa mwanamke mmoja… wanatarajia kupata mtoto

Spread the love

 

STORI za mapacha kushare au kuvaliana nguo, kusomea taaluma moja, kufanya kazi ya aina moja, kufunga harusi siku moja na wakati mwingine hata kufariki tarehe moja, ni moja ya mambo yaliyowahi kutokea katika maeneo mbalimbali duniani. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea). 

Katika visa vingine ambavyo pia ni nadra sana kutokea, ni mapacha wasichana kuolewa au kuwa katika uhusiano wa kimapenzi na mwanaume mmoja.

Lakini uamuzi wa ndugu mapacha wa kiume kuamua kuoa mwanamke mmoja ni jambo ambalo limegonga vichwa vya habari huko nchini Rwanda.

Tukio hilo limewaacha watu wengi vinywa wazi baada ya mapacha hao wa kiume kuishi kwa amani bila wivu na mwanamke mmoja.

Safari ya ndoa yao ilianza wakati mwanamke huyo aliyefahamika kwa jina la; Mary Josiane kujichanganya wakati akitoka kimapenzi na mmoja wa pacha hao.

Akisimulia mkasa huo wa kufurahisha, Josiane anasema wakati akianza safari ya uchumba na mpenzi wake hakuwahi kujua kuwa mwenzi wake alikuwa na ndugu yake ambayi ni pacha mwenzie. Hata kijana huyo hakuwahi kumweleza mpenzi wake yaani Josiane kuwa anaye ndugu yake ambaye ni pacha.

Utata ulianzia hapa…

Josiane anasema siku moja, alipotoka ‘out’ kupata chakula cha jioni ghafla alikutana na pacha mwingine ambaye hakuwa mpenzi wake, lakini Josiane aliamini ndiye yule mpenzi wake kwa kuwa walikuwa wamefanana kila kitu.

Anasema kwa kuwa hakufahamu chochote alimuonesha mapenzi kama yote kwa kumpokea kwa mabusu motomoto pamoja na kumkumbatia mithili ya watu wawili wapendanao.

Anasema hadi hapo pacha huyo ambaye hakuwa mpenzi wake, hakuonesha mshtuko wowote zaidi ya kuonesha ushirikiano wa kutosha licha ya kwamba pacha ndugu yake hakuwahi kumwambia kuwa ana uhusiano wao.

“Na hapo ndipo safari yetu kimapenzi na pacha wa pili ilipoanza,” anasema Josiane.

Anasema upendo wao uliongezeka hadi alipokuja kushtuka alipokutana na ndugu hao mapacha wote wawili.

“Sikuwa na la kufanya kwa sababu hata sikuweza kuwatofautisha.,” anasema.

Kwa kuwa mapenzi kati ya hao watatu yalishamiri, waliamua kufunga ndoa ya kimila.

Mwanadada huyo pia alifurahia uamuzi wa ndugu hao kumuoa na sasa wanatarajia kumpata mtoto wao wa kwanza hivi karibuni.

Lakini wanaishije?

Inaelezwa kuwa mapacha hao wamekubali kulala na mke wao kwa zamu. Kwamba wakati mmoja analala na Josiane mwingine analala kwenye chumba kingine peke yake ili kuepuka mgongano au wivu kati yao pindi wawapo kitandani.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Mawakili waiburuza mahakamani TLS, EALS

Spread the love  WAKILI Hekima Mwasipu na wenzake wawili, wamefungua kesi katika...

Habari Mchanganyiko

Uvuvi bahari kuu wapaisha pato la Taifa

Spread the love  SERIKALI imesema uvuvi wa bahari kuu umeliingizia Taifa pato...

Habari Mchanganyiko

DPP aweka pingamizi kesi ya ‘watu wasiojulikana’

Spread the love  MKURUGENZI wa Mashtaka nchini (DPP), ameweka pingamizi dhidi ya...

Habari Mchanganyiko

Washindi saba safarini Dubai NMB MastaBata ‘Kote Kote’

Spread the loveKAMPENI ya kuhamasisha matumizi ya Mastercard na QR Code ‘Lipa...

error: Content is protected !!