August 19, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mapacha walioungana vifua watenganishwa Muhimbili

Spread the love

HOSPITALI ya Taifa Muhimbili leo tarehe 1 Julai, 2022 imefanya upasuaji mkubwa wa kutenganisha watoto pacha waliozaliwa wameungana sehemu ya kifua, tumbo na ini (lakini kila mtoto ana ini lake), upasuaji huo umefanyika kwa saa saba na kuhusisha wataalam 31 ambao 26 kati yao ni watanzania na 5 kutoka ireland, akiwemo daktari mkuu wa upasuaji. Anaripoti Mwandishi Wetu… (endelea).

Upasuaji huo umekuwa wa kwanza wa aina yake nchini Tanzania, na wa tatu pekee kufanyika barani Afrika, huku upasuaji mwingine wawili ukifanyika Afrika Kusini na Misri.

Kwa mujibu wa uongozi wa hospitali hiyo upasuaji huo mapacha Rehema na Neema umegharimu takriban Sh milioni 50. Ambapo ungefanyika nje ya nchi ungegharimu zaidi ya Shilingi milioni 120.

Upasuaji huu mkubwa na wa kihistoria umekuwa sehemu ya jitihada za serikali ya Tanzania ambayo imekuwa ikipunguza mzigo wa gharama kwa Watanzania kwa kumudu kufanya upasuaji nyumbani, tofauti na nje ya Tanzania ambako gharama ni kubwa zaidi.

Kisa cha pacha hawa kinafananishwa na kisa cha pacha wengine walioungana waliogusa nyoyo za wengi nchini Tanzania Maria na Consolata.

Hata hivyo, hawakutenganishwa na waliishi wakiwa wameungana hadi walipofariki dunia tarehe 2 Juni mwaka 2018

 

error: Content is protected !!