July 6, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Maoni ya wananchi kufuatia hotuba ya Rais Jakaya Kikwete

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dr. Jakaya Kikwete

Spread the love

BAADA ya hotuba ya Rasi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dr. Jakaya Kikwete kupitia kwa Wazee wa Dar es Salaam, kulizuka mijadala mbalimbali huku kila mmoja akisema lake kutokana na alivyoielewa hotuba hiyo.

MwanaHALISI Online iliamua kuanzisha mada kupitia ukurasa wake wa Facebook, ikiwa na mada hii hapa chini,

Bila shaka ukiwa mmoja wa Watanzania waliomsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete. Una maoni juu hotuba na maamuzi yake kuhusu sakata la Escrow?

Maoni ya wasomaji katika ukurasa huo ni kama ifuatavyo:-

Man Masu Sijawahi kuona hotuba mbovu kama ile, hasa pale aliposema, kutaifisha IPTL kutafukuza wawekezaji.!!! Wakati huko watokako hao wawekezaji ndio waliositisha misaada hadi suala hili lichukuliwe hatua stahili. Rais anapaswa kupumzika. Huenda bado ni mgonjwa.

Bamdogo Kiki Mkuu tumabie kwanza kwa nini mwanahalisi forum haipatikani?

Boniface Mwaria Msarie naomba niwape summary ya kile alichosema. kwa kifupi angeweza kusema “BLAH BLAH BLAH BLAAAAH” na hiyo ikawa ndo hotuba yake

Vincenty Sr Edward Chumvi imechacha hawa CCM mchezo wao umefika mwisho kw kuwa rais kaamua kujifunga kitanzi mwenyewe anaxema pesa cyo za umma sasa kwa nini amemwondoa wazr w ardhi? Kama bunge lili kubali na kuridhishwa na uchunguzi yy anasubiri uchnguz w nini ili afanye maamuzi? Mim nashauri kwenye vikao vijavyo wapige kura y kutokuwa na imani na rais Over.

Glove Mdeya ilikuwa hotuba ya chama sasa tunasubiri akiwa kama rais wa nchi

Hamadi Bakari Hotuba imetupa maswali zaidi !!!! Hajamaliza kiu yakuona kweli rais anchukizwa na rushwa , hata pale ukumbini alivyotaja kumuondoa mama tibaijuka watu walilipuka inaashiria walitarajia na Mengi zaidi

Cosmas Aloyce Wale wazee walikunja sura walipoona hotuba inafika tamati ndio mh akaona hapa pagumu akamtoa Ana sadaka ila ccm Kuna kulindana.

Esther Venance Mdee hotuba yake ilikuwa imekaa kimzaha japo alichukua maamuzi ya kumuweka pembeni mama Tibaijuka. pia inatia mashaka kama kweli hizo mamlaka za TAKUKURU na Tume ya maadili ya utumishi wa umaa endapo wataweza kutoa kufanya kazi yao vizuri kwa hao wanaowashughulikia na kuwahoji.

Evernder Josephat Mi naona Rais analalamika kama ninavyolalamika mimi….

Onesmo Thomas Porojo tupu! Kama fedha sio za serekali Tibaijuka kakosa nini? Hivi kuweka MTU kiporo na uchunguzi ulishabainisha kosa lake ni kutufanya sisi wananchi mazuzu sio!

Kanani Chombala mlitaka nini zaidi kwa mzaramo? chaguen masai muone kazi hammkumbuki sokoine??

Hance Senior Kapiga porojo kaenda zake

Fabiance Kweka mimi Maoni yangu naona watz hauotuongozwi na serikali tunaongozwa na mungu maana nchi yenyewe haiongozwi tena na katiba tunaongozwa na mawazo ya wazee wa dsm, kwani mm kama mtanzania rais hakwenda kutoa maamuzi alienda kutoa ufafanuz ambao hatukuuhitaji, hivyo kipekee naona kama kachemka na amewaona watanzania wapumbavu.

Yunusa Nzomukunda bullshit.

Muddy Montanna Jr. MAAJABU YANAENDELEA TANZANIA

Kizito Shio Aloyce mgawo ulimpitia ndo maana anawalinda wezi wenzake.

John Victory Hajatatua tatizo kwan alichofanya ni kuongeza tatizo na nilichokiona ni alikuwa anazoza tu na kuwatetea wezi, viongozi walioshindwa kutekeleza majukumu yao na pia kuitetea IPTL na kwa hali hiyo umasikin kuondoka Tz ni ndoto na maisha bora kwa kila mtan

Kelvin Nicholaus Amekuwa wakili wa IPTL na PAP…..Imesikitisha sana na kukatisha tamaa.

Mpella Sylvenus kwanza hana nidhamu kwa wananchi wake. kutuambia sisi ni watu wa KUZOZA TU hakututendea haki tuliyempa dhamana ya kulinda rasilimali zetu. kumbe ndo maana mbuga yetu ya Serengeti ameibinafsisha ni dlili tosha keshauza huyu jamaaa.

Fadhili Khalfani Mm nafikili raisi anafurahia ufisadi unafanyika ndani ya serikali yk ndio mana jana hotuba yk haikuwa na jipya.

Erasto Kalinga Yeye ndio aliyepata mgao mkubwa.

Amiry Swaleh siku zote mwizi huwez kumhukum mwizi mwenzake

Pancras Vitalis ile xio hotuba ya kuxikilizwa na m2 mwenye akili.

Jumanne Zeddy Changa la macho tu.

Jitu La Mungu ndio wale wale kawaida yake kuandikiwa hotuba pumba na yeye kuzisoma wakati mwenyewe yumo kwenye dili.

Sule Babuwazir Hamad Bakari umenena kaka. Watu walichokipigia vigeregere mwishoni ndicho walichokua wakikitamani kifanyike tangu mwanzoni.

Abdallah Mbanga Haijanifurahisha. Kabisa kaficha ficha mambo.

Revocatus Morand Kanichefua eti hela ya madafu!!!.

Abdallah Simba Tatizo anaendesha nchi kishkaji sana mimi sijamuelewa kabisa anatuharibia CCM yetu.

Dani Stephen ciyo poa kwasabu kaficha baadhi ya ukweri.

Huruma Mwampashi Kama kawaida badhi ya watu wamelindwa kama kawaida.

Douglas Mgeni Kuna vitu havikuwekwa waz katka hotuba

Kidunda Ramadhani Kuna haja bunge kuongezewa mamlaka hasa kwenye maamuzi.

James Mengo Hotuba ya kitoto na nasikitika sikuingia darasani kwa ajili yake nikaambulia 0

 

error: Content is protected !!