January 23, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Maombi ya majimbo mapya Mei 31

Kaimu Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Kalima Ramadhani akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya utaratibu wa kugawa majimbo

Spread the love

TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), imesema kuwa, kati ya tarehe 13 Mei hadi 31 mwaka huu, ndio muda uliotengwa kwa ajili ya kupokea mapendekezo ya ugawaji wa majimbo. Anaandika Sarafina Lidwino…(endelea).

Kaimu Mkurugenzi wa NEC, Kailima Ramadhani, amewaeleza waandishi wa habari leo kwamba, takwimu za idadi ya watu zitakazotumika ni za makisio mpaka mwaka 2015 na zitapatikana Ofisi ya Takwimu ya Taifa.

Amesema kwa mujibu wa takwimu “Population quota”, kwa upande wa majimbo ya mijini itakuwa 325,000 na kwa majimbo ya vijijini ni 235,000, hivyo kuyataka majimbo ambayo hayajatimiza idadi hiyo ya watu wasilete maombi isipokuwa tu kama ni halmashauri mpya.

Ramadhani amefafanua kuwa, vigezo vitakavyotumika katika ugawaji huo ni idadi ya watu, ambapo watazingatia ongezeko la watu  hadi kufikia Julai mwaka huu, upatikanaji wa mawasiliano, ambapo watazingatia uwepo wa miundombinu kama barabara.

Vigezo vingine ni hali ya kijiografia, ambapo litaangaliwa jimbo lipo sehemu gani kama ni mlimani au bondeni, mazingira ya muungano, uwezo wa ukumbi wa Bunge na viti maalumu vya wanawake ambapo watatenga kiasi cha zaidi ya asilimia 30 kwa ajili ya wabunge wanawake.

Amesema, watazingatia hali ya kiuchumi kwa kushirikisha Tamisemi, ukubwa wa eneo, mipaka ya kiutawala, jimbo moja lisiwe ndani ya wilaya au halmashauri mbili, kata moja isiwe ndani ya majimbo mawili na mpangilio wa maeneo ya makazi ya watu yalipo.

Kwa mujibu wa Ramadhani, utaratibu utakaotumika kuwasilisha maombi hayo ni wananchi kuwasilisha maoni yao kwa Mkurugenzi wa halmashauri husika, kisha halmashauri itayawasilisha kwa Katibu Tawala wa Mkoa (RAS).

Amesema baada ya hapo RAS atawasilisha maombi katika kikao cha kamati ya ushauri ya mkoa (RCC) ili kupata maoni zaidi. Kwamba, baada ya hapo yataletwa NEC na kuanza kufanyiwa kazi.

error: Content is protected !!