Friday , 3 February 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Maombi ya kutafuta uhuru wa Mbowe yashika kasi Chadema
Habari za Siasa

Maombi ya kutafuta uhuru wa Mbowe yashika kasi Chadema

Spread the love

 

WANACHAMA na wafuasi wa Chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania-Chadema, wameendelea kufanya maombi maalum, ya kumsihi  Mungu aingilie kati kwenye kesi inayomkabili mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe, na wenzake.Anaripoti Mwandishi Wetu, Mwanza…(endelea).

Mbowe na wenzake, Halfan Bwire Hassan, Adam Hassan Kasekwa na Mohammes Abdillah Lingwenya, wanakabiliwa na  Kesi ya Uhujumu Uchumi, iliyopo kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu. Kwa sasa mwanasiasa huyo na wenzake wako mahabusu ya Gereza la Ukonga, jijini Dar es Salaam.

Leo Jumapili, tarehe 8 Agosti 2021, wanachama wa Chadema Kanda ya Victoria, wamefanya maombi katika Kanisa Katoliki Bugando, jijini Mwanza, wakiomba rehema ya Mungu,  ili Mbowe na wenzake watatu waachwe huru.

Akizungumza baada ya maombi hayo,  Katibu wa Kanda ya Victoria,  Zacharia Obad, amesema njia pekee itakayomuweka huru Mbowe na wenzake,  wanaokabiliwa na mashtaka ya kula njama za kufanya ugaidi, ni maombi.

Freeman Mbowe akiwa mahakamani Kisutu

“Leo tumefika kanisani  kwa ajili ya kusali misa, ambayo ilikuwa lengo letu kwa muda mrefu toka mwenyekiti na viongozi wengine walivyokamatwa. Nia yetu Mungu aingilie kati, haki itendeke.  Pia Watanzania tuungane maana tunahitaji Serikali inayotenda haki,  isibambikie kesi watu,” amesema Obad.

Obad amesema kuwa, wamemuomba Mungu, awajaalie Watanzania moyo wa kupendana badala ya kuishi kwa visasi.

“Lakini tunamuomba Mungu aingilie kati,  awajaalie Watanzania wote moyo wa kupendana na kujaliana, hatuhitaji roho za chuki,  tutaenda hivyo kwenye msikiti, kwa wa sababo ili kuhakikisha maombi yanafanyika,” amesema Obad na kuongeza:

“Wanachama wengi wameingia kwenye misa na wengine hawakuvaa sare za chama sababu lengo sio kuvaa sare,  lengo ni namna gani watu wameguswa. Tumeona tulivyofanya majitoleo waumini walipiga makofi,  inaonesha Watanzania wanataka amani zaidi,  hawataki mambo ya kubambikiana kesi, hakuna watu wenye hati miliki ya Tanzania,  hati miliki ni ya wote.”

Wanachama hao walifika kanisani hapo wakiwa na sare za Chadema, huku wengine wakivaa nguo za kawaida.

Hii sio mara ya kwanza kwa wafuasi wa Chadema kufanya maombi hayo, kwani hivi karibuni baadhi yao walifanya maombi maalum jijini Mwanza, yaliyoongozwa na Askofu wa Kanisa la Evangelical Pentecostal Restoration (ERPC), Amos Hulilo.

Mbowe anasota mahabusu tangu tarehe 21 Julai 2021, alipokamatwa jijini Mwanza kisha kuhamishiwa jijini Dar es Salaam. Huku wenzake wakisota tangu Agosti 2020.

1 Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Kamati ya Bunge yaitaka Serikali kuchunguza dawa za asili

Spread the love  KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo...

Habari za Siasa

Kada NCCR-Mageuzi aliyepotea aokotwa porini akiwa taabani, hajitambua

Spread the love  MWENYEKITI wa Jumuiya ya Vijana ya Chama cha NCCR-Mageuzi,...

Habari za Siasa

ACT Wazalendo yataka Jaji Mkuu, Jaji Biswalo wajiuzulu kupisha uchunguzi fedha za Plea Bargaining

Spread the love  CHAMA cha ACT-Wazalendo, kimemtaka Jaji wa Mkuu wa Tanzania,...

Habari za Siasa

Kigogo ACT-Wazalendo: Vyama vya upinzani vilikosea kumpokea Membe, Lowassa

Spread the love  KATIBU Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo, Ado Shaibu, amesema...

error: Content is protected !!