October 18, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Maofisa wanne wa jeshi la Rwanda wauawa Msumbiji, 14 wajeruhiwa

Rais Filipe Nyusi wa Msumbiji

Spread the love

 

MAOFISA wanne wa jeshi la Rwanda wameuawa nchini Msumbiji, katika operesheni ya kijeshi dhidi ya wanamgambo wa kiislamu, katika jimbo la Cabo Delgado. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Taarifa kutoka nchini Rwanda zinasema, wanajeshi wengine 14, wamejeruhiwa vibaya katika mapigano hayo.

Hii ni mara ya kwanza kwa Rwanda kutangaza majeruhi katika kikosi chake cha wanajeshi 1,000 kilichopo nchini Msumbiji, tangu waanze operesheni ya kukabiliana na wanamgambo hao.

Haijawekwa wazi ni katika eneo gani haswa la jimbo la Cabo Delgado, ambako wanajeshi wa Rwanda waliuawa.

Jumamosi iliyopita, marais wa Msumbiji – Filipe Nyusi na wa Rwanda, Paul Kageme – waliwapongeza wanajeshi ambao wamejitoa kupambaa na magaidi.

Rwanda imepeleka nchini humo wanajeshi 1,000 kukabiliana na wapiganaji hao wanafanya mashambulizi ya uharibifu kaskazini mwa taifa hilo.

Wapiganaji hao, wameteka eneo muhimu lenye barabara ya makutano, ambalo lilikuwa likishikiliwa na wapiganaji hao kwa zaidi ya kipindi cha mwaka mmoja uliopita, na wamefika katika mji muhimu wa Mocimboa da Praia.

Katika kipindi cha miaka minne wapiganaji hao walichukua udhibiti wa wilaya tano muhimu katika mkoa wa Cabo Delgado katika eneo la Mashariki la Msumbiji.

Kufikia sasa takribani watu 3,100 wameuawa na wengine 820, 000 kuwachwa bila makao.

Wakati makundi ya uasi yalipoteka mji wa Palma mwezi Machi, mji wenye utajiri wa gesi ambako kunatengenezwa kiwanda chenye thamani ya dola bilioni 20 (£14bn) kikiwa ni kiwanda cha pili kwa ukubwa barani Afrika, kampuni ya Ufaransa ya mafuta ililazimika kuacha ujenzi mkubwa katika eneo hilo.

Jeshi la ulinzi la Msumbiji linafahamika kwa kiasi kikubwa kuwa ni lenye ufisadi, lenye mafunzo ya kiwango cha chini na lenye ukosefu wa vifaa na kwamba wasingeweza kukabiliana na mashambulio ya wapiganaji.

Mwamko wa uasi ulianzishwa na vijana wasio na ajira wanaopinga kuongezeka kwa umasikini na ukosefu wa usawa, pamoja na ukosefu wa faida zitokanazo na raslimali ikiwa ni pamoja na gesi na mawe ya thamani ya rubi.

Mzozo katika eneo la Kaskazini mwa Msumbiji, ulioanza na shambulio dhidi ya Mocímboa da Praia mwaka 2017, umewalazimisha zaidi ya watu 800,000 kukimbia makazi yao.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka maeneo hayo, mzozo huo ukaendelea kuwa mbaya kufuatia hatua ya vijana kuteka silaha na kupata uungaji mkono wa wenyeji.

Waasi hao wanaojiita “al-Shabab,” jina ingawa hawana uhusiano na kundi lenye jina sawa na hilo nchini Somalia.

Eneo lenye mzozo linakaliwa na Waislamu wengi, na kufikia mwaka 2019 waasi walikuwa wamewasiliana na kundi la Islamic State (IS).

Rwanda imejenga mahusiano na Israeli, ambayo bila shaka ingeunga mkono harakati dhidi ya IS.

Marekani imewapatia jina la “Isis Mozambique” na kuwataja kama shirika la kigeni la ugaidi.

Vijana wavuvi wa Msumbiji walirejea kwenye mwambao baada ya siku kadhaa za uvuvi katika Palma, ambako hifadhi kubwa ya gesi asilia ilipatikana kwenye mwambao, tarehe 16 Februari 2017.

Watu wengi hutegemea uvuvi kujikimu kimaisha kaskazini mwa Msumbiji.

Kikundi cha kimataifa cha masuala ya mizozo (IGC), kimesema hivi karibuni, kwamba wapiganaji wana “uhusiano dhaifu” na kwamba “sababu halisi inaochochea mzozo huu ni kuhusu malalamiko ya wenyeji.”

Ureno, ambayo ni koloni la zamani, pamoja na Marekani tayari wana wanajeshi wao nchini Msumbiji wanaotoa mafunzo kwa wanajeshi wa Msumbiji ili kupigana na makundi ya uasi.

error: Content is protected !!