Tuesday , 16 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Maofisa wa madini, wakuu wa mikoa kushirikiana kulinda madini
Habari MchanganyikoTangulizi

Maofisa wa madini, wakuu wa mikoa kushirikiana kulinda madini

Madini ya dhahabu
Spread the love

WAZIRI Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa, ametoa maelekezo kwa Maofisa madini kote nchini kunakochimbwa madini kushirikiana na wakuu wa Mikoa kwa lengo la kuweka mikakati ya kuthibiti madini hayo yasitoroshwe. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Majaliwa ametoa maelekezo hayo jana wakati wa ufunguzi wa Mkutano kuhusu uanzishwaji wa masoko ya Madini, uliofanyika Jijini Dodoma.

Katika mkutano huo uliowahusisha, wakuu wa Mikoa, matibu tawala, manaibu matibu wakuu na maofisa wa Madini Majaliwa aliwataka viongozi hao kufanya kazi kwa kushirikiana kwa lengo ya kufanya kazi yenye tija kwa lengo la kulinda rasilimali za nchi. 

Kiongozi huyo alisema kuwa kila mkuu wa mkoa ambako kunachimbwa madini anatakiwa kufanya kazi kwa kushirikiana na maofisa madini kwa kuona ni namna gani ya matumizi bora ya kanuni ya uanzishwaji wa masoko.

Mbali na hilo Majaliwa amekemea baadhi ya vitendo vya baadhi ya watumishi wa serikali kutofautiana wao kwa wao au kutofaitiana na wawekezaji badala ya kutumia njia njia bora ya kutatua migogoro.

Naye Waziri wa Nishati na Madini, Dotto Biteko katika mkutano huo alisema kuwa ili kukabiliana na Changamoto ya Masoko ya Madini Wizara ya  Madini iliunda kamati iliyojumuhisha wajumbe kutoka katika taasisi mbalimbali za kiserikali zikiwemo Ofisi ya Rais Ikulu Ofisi ya Rais Tamisemi Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali Wizara ya Madini.

Ofisi nyingine ni Wizara ya Fedha Wizara ya Viwanda na Biashara, Benki Kuu na Tume ya Madini na tume hiyo iliundwa ili kuandaa rasimu ya kanuni za kuanzisha na kusimamia masoko ya madini nchini.

Kwa upande wake Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, (TAMISEMI), Selemani Jaffo amewataka wakuu wa mikoa kuhakikisha wanafanya kazi zao kwa umakini na kwa muda badala ya kusuasua.

Akizungumzia suala la ugawaji wa vitambulisho vya wajasiliamali Jafo alisema kuwa bado ipi baadhi ya mikoa ambayo mpaka sasa haijafanya vizuri katika utoaji wa vitambulisho vya wamachinga jambo ambalo si zuri.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Samia arejesha mikopo ya 10%, bilioni 227.96 zatengwa

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amerejesha utaratibu wa utoaji mikopo...

Habari Mchanganyiko

Sekta binafsi yasifu utekelezaji wa Mkumbi

Spread the loveSERIKAL imepongezwa kwa utekelezaji wa mapendekezo ya sekta binafsi kupitia...

Habari Mchanganyiko

Kamati ya bunge yapigia chapuo kilimo ikolojia

Spread the loveSERIKALI kupitia Wizara ya Kilimo imeshauriwa kushirikiana na wadau wa...

Habari Mchanganyiko

Serikali yapata hasara 113 milioni hospitali kuwapa misamaha wagonjwa wasiostahili

Spread the loveSERIKALI imepata hasara ya kiasi cha Sh. 111.76 milioni, baada...

error: Content is protected !!