Friday , 29 March 2024
Home Habari Mchanganyiko Maofisa ulinzi, usalama watakiwa kutumia mbinu mbadala kudhibiti ukiukwaji ukatili kijinsia
Habari Mchanganyiko

Maofisa ulinzi, usalama watakiwa kutumia mbinu mbadala kudhibiti ukiukwaji ukatili kijinsia

Spread the love

MAOFISA wa vyombo vya ulinzi na usalama vinavyodhibiti masuala ya ukiukwaji wa haki za binadamu na ukatili wa kijinsia, wametakiwa kutafuta njia mbadala za kudhibiti makosa hayo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Mratibu wa THRDC, Onesmo Olengurumwa

Wito huo umetolewa leo tarehe 17 Agosti 2022 katika mafunzo ya kuwakumbusha misingi ya haki za binadamu na changamoto za ukatili wa kijinsia kwa maofisa wa vyombo vya dola yaliyoandaliwa na Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) kwa kushirikiana na Shirika la CISEMA, jijiji Dar es Salaam.

Akizindua mafunzo hayo, Kamishina wa Polisi Jamii (CP), Fausitine Shilogile ambaye amemuwakilisha Mkuu wa Jeshi la Polisi, (IGP) Camilius Wambura amesema matukio hayo yamongezeka na kwamba maofisa hao wanapswa kutumia mafunzo kutafuta namna ya kuyadhibiti.

Kamishina wa Polisi Jamii (CP), Fausitine Shilogile

“Matukio ya unyanyasaji wa kijinsia yamekuwa yakiongezeka kila siku hata katika taarifa zetu huwezi kukosa tukio la kubaka, kulawiti na makosa mengine ya namna hiyo. Sasa kwa nini yanaongezeka tutajifunza katika semina hii na kubadilishana mawazo mbalimbali kulingana na maeneo yetu tunayotoka na utendaji wa makosa na namna gani ya kuyashughulikia,” amesema CP Shilogile.

Naye Mkurugenzi Msaidizi kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP), Renatus Mkude amewataka maofisa hao watafute njia mbadala ya kudhibiti makosa hayo badala ya kuishia kuwakamata na kuwafikisha mahakamani peke yake.

“Sehemu nyingine tunayopaswa kuangalia ni namna ya kushughulikia na makosa haya, sisi ofisi ya DPP tumekuja na engagement ya aina hiyo ya kuwapeleka maofisa sehemu nyingine kujifunxa, tutumie nafasi hii kushirikishana uzoefu haya mambo ya kupinga ukatili wa kijinsia yako mengi sana ni vizuri tuweze kuyawekea mkakati ili mwisho wa siku tuyatokomeze kabisa,” amesema Mkude.

Kwa upande wake Mratibu wa THRDC, Onesmo Olengurumwa amewataka maofisa wa vyombo vya ulinzi na usalama kuwashirikisha zaidi wananchi katika kukabiliana na vitendo hivyo kwa kuwa wao wana taarifa za watuhumiwa wanaovitekeleza.

“Sehemu ya msingi katika kupambana na vitendo vya ukatili wa kijindia ni ufuatiliaji wa taarifa toka kwa wananchi. Tunasisitiza kabisa tuendelea kufanya kazi kwa pamoja tukishirikiana wananchi watatuelewa na kutusaidia kuona haki zinalindwa sababu wanaovunja haki ni wananchi lakini jeshi hamuwezi kuzuia wenyewe bila kushirikiana na sisi wadau,” amesema Olengurumwa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

DAWASA waanza utekelezaji agizo la Samia

Spread the loveMamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam...

Habari MchanganyikoKimataifa

Zuma akataliwa kugombea urais

Spread the loveTUME Huru ya Uchaguzi Afrika Kusini (IEC) imemwondoa rais wa...

Habari Mchanganyiko

Mtandao watetezi wa haki za mazingira Tanzania waundwa

Spread the loveMTANDAO wa watetezi wa haki za mazingira nchini Tanzania, umeundwa...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kapinga kuongoza usambazaji wa mitungi ya gesi 10,000 ya Taifa Gas

Spread the loveNaibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga ameahidi kuongoza kwa ufanisi...

error: Content is protected !!