August 16, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Maofisa madini watakiwa kujituma

Spread the love

MAOFISA madini kutoka Wizara ya Nishati na Madini nchini wametakiwa kujituma na kuwa wazalendo wa nchi yao, anaandika Christina Raphael.

Kufanya hivyo kunaelezwa kutasaidia kukusanya mapato ya tozo na kodi za leseni kwa mfumo wa mtandao ili kuifanya wizara kuwa na ongezeko la uchangiaji katika Pato la Taifa kutoka asilimia 3.5 iliyopo hadi asilimia 10 ifikapo mwaka 2025.

Profesa James Mdoe, Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini amesema hayo leo wakati akifungua mafunzo kwa mfumo wa mtando kwa watumishi wa wizara hiyo yaliyofanyika kwenye Chuo Kikuu cha Kilimo cha (SUA) mkoani Morogoro.

Amewataka maofisa hao kutumia mbinu mbalimbali ili kuhakikisha wanakabiliana na changamoto zilizopo za matumizi ya mtandao na kufanikisha utoaji leseni za madini unafanyika kwa mfumo wa mtandao na kuachana na matumizi ya karatasi.

Bertha Luzabiko, Kaimu Kamishna wa Madini Mkoa wa Morogoro amesema, mafunzo hayo ya wiki mbili kwa maofisa hao yanafanyika ili kuboresha huduma za leseni kwa mfumo wa mtandao.

Amesema, mafunzo hayo ni muendelezo wa maboresho ya wizara kufuatia mabadiliko ya sera ya kukuza uchumi na kufanya kasi ya uwekezaji katika sekta ya madini kuongezeka.

error: Content is protected !!