July 1, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Maofisa 77 Magereza wavishwa vyeo

Mkuu wa Jeshi la Magereza, Kamishina Jenerali, John Minja akimvisha cheo Mrakibu wa Magereza, A. Lusenene kuwa Mrakibu Mwandamizi wa Magereza

Spread the love

KAMISHNA Jenerali wa Jeshi la Magereza (CGP), John Minja amewavisha vyeo maofisa wa magereza 77 wa mkoa wa Dar es Salaam kati ya 292 waliopandishwa nchi nzima. Anaandika Pendo Omary… (endelea).

Shughuli hiyo imefanyika leo katika viwanja vya Chuo cha Maofisa Ukonga, ikiwa ni utekelezaji wa maamuzi ya kikao cha Tume ya pamoja ya Polisi na Magereza.

Kikao hicho kilifanyika 16 Machi mwaka huu, mjini Dodoma, ambapo jumla ya maofisa magereza 292 walipandishwa vyeo nchi nzima.

Akizungumza baada ya kuwavisha vyeo maofisa hao, Minja amesema “kuteuliwa kwao kulizingatia uzoefu kazini, nidhamu na utendaji mzuri”.

“Vigezo vingine ni elimu, ujuzi na jinsia ambapo kati ya maofisa 292 waliopandishwa vyeo nchini nzima wanawake ni 37 sawa na asilimia 13. Idadi ya wanawake ni ndogo lakini tumeanza kuwapandisha maafisa wa vyeo vya chini ili kuleta uwiano unaotakiwa,” amesema Minja.

Aidha, vigezo vingine vilivyozingatiwa ni: uwezo wa kumudu madaraka zaidi na kuwepo kwa nafasi kwa cheo husika.

Akizungumzia kuhusu matarajio ya Magereza kwa maofisa hao, Minja amesema “wanapaswa kuongeza ari ya utendaji kazi kwa bidii na kazi yenye viwango”.

“Pia tunatarajia muwe wabunifu, kuongoza walio chini yenu kwa vitendo, kuacha kufanya kazi kwa mazoea na kujiendeleza kielimu ili kuweza kupanda madaraka zaidi,” amesema Minja.

Tume ya pamoja ya Jeshi la Polisi na Magereza iliazimia warakibu waandamizi wa Magereza (SSP) 11 kuwa makamishna wasaidizi (ACP).

Aidha, mrakibu wa magereza (SP) 41 kuwa warakibu waandalizi (SSP) na warakibu wasaidizi wa magereza (ASP) 83 kuwa warakibu wa magereza (SP).

Pia wakaguzi wasaidizi wa magereza (A/I) 152 kuwa wakaguzi wa magereza (Inspekta).

Amesema kuwa maofisa hao 77 ni kwa niaba ya wenzao 292 kwa kuwa hawezi kuwavisha wote nchini nzima kwa wakati mmoja.

error: Content is protected !!