Saturday , 20 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Maofisa 4 NEMC mbaroni tuhuma za utakatishaji fedha
Habari Mchanganyiko

Maofisa 4 NEMC mbaroni tuhuma za utakatishaji fedha

Afisa Uhusiano wa Takukuru, Doreen Kapwani
Spread the love

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), inawashikilia watumishi wanne wa Baraza la Taifa la Uhifadhi wa Mazingira (NEMC) kwa tuhuma mbalimbali ikiwemo makosa ya rushwa na utakatishaji fedha. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Watuhumiwa hao, wanashikiliwa katika ofisi za Takukuru, Upanga jijini Dar es Salam na kesho Alhamisi tarehe 4 Juni 2020 watafikishwa mahakamani.

Taarifa ya Afisa Uhusiano wa Takukuru, Doreen Kapwani aliyoitoa leo Jumatano tarehe 3 Juni 2020 imesema, watuhumiwa hao wamekuwa wakichunguzwa kwa makosa mbalimbali na uchunguzi huo umekamilika.

Amewataja watuhumiwa hao ni; Deusdedith Katwale, Magori Matiku na Obadia Machupa ambao wote ni maafisa mazingira na Lydia Nyinondi ambaye ni Mhasibu Msaidizi. Wote wa makao makuu.

Doreen ametaja tuhuma zao ni; kula njama na kutenda kosa, kughushi, kuwasilisha nyaraka za uongo, kuisababishia mamlaka hasara, matumizi mabaya ya madaraka pamoja na utakatishaji wa fedha haramu.

“Tunapenda kuujulisha umma pia, Takukuru kwa kushirikiana na ofisi ya taifa ya mashtaka inatarajia kuwafilisha watuhumiwa hawa mahakamani kesho tarehe 4 Juni 2020,” amesema Doreen

Katikati hatua nyingine, Doreen amesema, Takukuru inamshikilia Eliud Kijalo ambaye ni Afisa wa wizara ya maliasili na utalii kwa makosa ya ubadhirifu wa zaidi ya Sh. 4 bilioni.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wauguzi, madaktari 1000 kugawiwa mitungi ya Oryx Gas

Spread the loveKAMPUNI ya Oryx Gas na Taasisi ya Doris Mollel Foundation...

Habari Mchanganyiko

Tanzania yachaguliwa Makamu wa Rais Tume ya Shirika la Hali ya Hewa Duniani

Spread the love  TANZANIA kupitia Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA)...

Habari Mchanganyiko

NEMC yaonya wanaojenga bila tathmini ya mazingira

Spread the loveBARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC),...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB Pesa Akaunti yawavutia wakaguzi wa ndani Afrika

Spread the loveUbunifu wa bidhaa bora wa Benki ya NMB pamoja na...

error: Content is protected !!