CHAMA tawala cha China (CCP), kimewaadhibu zaidi ya maofisa 110,000, katika mapambano ya ufisadi. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa … (endelea).
Kwa mujibu wa kituo cha mawasiliano ya kimkakati cha Indo-Pacific (IPCSC) chama hicho cha kikomonosti kimewaadhibu maofisa hao baada ya kuchunguzwa hadharani.
Rais wa China Xi Jinping alizindua kampeni ya kupambana na ufisadi ambapo maafisa waliochunguzwa ni pamoja na maafisa wa ngazi za juu serikalini, wajumbe wa tume ya kijeshi, maafisa wa ngazi ya mawaziri, na mamia ya maafisa wa ngazi ya naibu waziri.
Katika robo ya kwanza ya mwaka huu watu 111,000 walitozwa faini, wakiwamo kada 633 ya mkoa, kada 669 ngazi ya wilaya na vitongoji 1,000. Inajumuisha kada za ngazi, na kada za jumla 15,000. Na watendaji 76,000 katika maeneo ya vijijini, mijini na sehemu za biashara.
Hayo yanaibuka wakati Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China ikitoa ripoti yao ya kila mwezi ya kupinga ufisadi.
Kamati hiyo ilitaja kuwa katika robo ya kwanza wakala wa ukaguzi na usimamizi wa nidhamu walipokea maombi na ripoti 776,000, ambapo 231,000 zilikuwa ni malalamiko na tuhuma.
Maafisa mashuhuri wanaochunguzwa ni pamoja na Du Zhaocai na Li Xiaopeng.
Taarifa zinaeleza kuwa ripoti ya Machi dhidi ya ufisadi ilisema kuwa ukiukaji 7,021 ulichunguzwa na kushughulikiwa. Hizi zilihusisha maafisa 10,285.
Leave a comment